WATU WANE WAUAWA NDANI YA KANISA KENYA


likoniattack_99d84.jpg
Watu wane wameuawa baada ya watu waliojihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi ndani ya kanisa karibu na mji wa bandari ya Mombasa nchini kenya.
Watu wengine kumi na saba wamejeruhiwa.
Maafisa wa polisi katika wilaya ya Likoni ambayo iko kusini mwa Mombasa wamesema kuwa majambazi hao walilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo kufuatia kutiwa mbaroni kwa watu wawili siku ya Jumatatu ambao polisi wanadai walikuwa wakimiliki mabomu yaliofichwa ndani ya gari yao.
Kumekuwa na visa tofauti vya ghasia mjini Mombasa katika miezi ya hivi karibuni vinavyoshirikisha vikosi vya usalama na Waislamu wenye itikadi kali.
Previous
Next Post »