MATOKEO YA MECHI YA REAL MADRID NA BARCELONA 4-3 REAL

Lionel Messi akiibusu nembo ya jezi ya Barcelona baada ya kufunga bao la ushindi katika El Clasico
MSHAMBULIAJI Lionel Messi amepiga hat-trick usiku huu Barcelona ikishinda 4-3 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.
Andres Iniesta alianza kuifungia Barcelona dakika ya saba, Karim Benzema akaisawazishia Real dakika ya 20 na kufunga la pili dakika ya 24.
Barcelona ikazinduka na kupata bao la kusawazisha dakika ya 42 kupitia kwa Messi, lakini Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo akaifungia Real bao la tatu dakika ya 55 kwa penalti.

Matchwinner: Messi points to the Barcelona support as Gerard Pique (centre) and Alexis Sanchez catch up
Messi akiwanyooshea kidole mashabiki wa Barcelona baada ya kufunga, huku Gerard Pique (katikati) na Alexis Sanchez wakimfuata
Flying high: Sergio Ramos celebrates Madrid's third with Ronaldo (left) while the Madrid star jumps for joy (right)
Flying high: Sergio Ramos celebrates Madrid's third with Ronaldo (left) while the Madrid star jumps for joy (right)
Sergio Ramos akishangilia bao la tatu la Madrid na Ronaldo (kushoto) wakati nyota huyo wa Madrid anaonekana akiruka kuliav>Messi akafunga mara mbili mfululizo kwa penalti dakika za 65 na 84 kukamilisha hat trick yake Barcelona ikifufua matumaini ya kutetea ubingwa wake msimu huu. Real Ilimpoteza beki wake Sergio Ramos aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 63 kwa kumuangusha Neymar kwenye eneo la hatari, wakati Pepe, Di Maria, Alonso, Modric na Ronaldo wote walionyeshwa kadi za njano na kwa upande wa Barcelona, Fabregas na Busquets pia walionywa kwa kadi za njano. Kwa matokeo hayo Real inabaki na pointi zake 70, ingawa inaendelea kuongoza La Liga kwa wastani wa mabao, ikiwa inalingana pointi na Atletico Madrid, ambayo mapema iliifunga Real Betis 2-0, mabao ya Gabi dakika ya 58 na Diego Costa 64, wakati Barcelona inabaki nafasi ya tatu licha ya kufikisha pointi 69. Barca na Real zimecheza mechi 28 kila moja, wakati Atletico imecheza mechi moja zaidi.    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Pepe, Ramos, Cristiano Ronaldo, Benzema/Varane dk64, Bale, Marcelo, Xabi Alonso, Carvajal, Modric/Morata dk90 na Di Maria/Isco dk85.  Barcelona: Valdes, Alves, Piqué, Mascherano, Jordi Alba, Sergio, Xavi, Iniesta, Fabregas/Sanchez, dk78, Messi na Neymar/Pedro dk69.
All square: Barcelona frontman Lionel Messi equalises for the Catalans minutes before the half-time whistle
Lionel Messi akifunga katikati ya msitu wa wachezaji wa Real
Floored: Javier Mascherano and goalkeeper Victor Valdes are left on their knees following Benzema's strike
Javier Mascherano na kipa Victor Valdes wakiwa chini, huku Benzema akitimka kushangilia baada ya kufunga
Man of the moment: Karim Benzema celebrates after equalising for Madrid following Barcelona's opener
Karim Benzema amefunga mabao mawili
Head-to-head: France international Benzema outleaps Mascherano to put Real Madrid into the lead
Benzema akigombea mpira wa juu na Mascherano
Altercation: Neymar looks on as Pepe lets his anger show by shouting into the face of Fabregas

Neymar akiwatazama Pepe na Fabregas wakifanyiana ubabe
Fallen: Fabregas and Pepe both ended up on the deck after their coming together and were booked
Fabregas na Pepe wote waliishia kuanguka na wote wakaonyeshwa kadi za njano 
Toe-to-toe: Bale stretches in a bid to retain possession as he is tackled by Barcelona goalscorer Iniesta
Bale akipambana na Iniesta
Grounded: Cristiano Ronaldo claims to have been fouled and appeals for a free-kick early on
Cristiano Ronaldo akilalamika baada ya kuchezewa rafu
Made in heaven: Two Real Madrid fans show their appreciation for star man Cristiano Ronaldo
Mashabiki wawili wa Real Madrid wakiwa na bango la kumtukuza Cristiano Ronaldo "Ameumbwa peponi".

Previous
Next Post »