Washiriki wa ‘Maisha Plus Rekebisha’ kutoka Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda wako Moro




kipanya

Mratibu wa shindano la Maisha Plus, Ally Masoud Kipanya.
WASHIRIKI wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika kwa jina la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchini Kenya, Rwanda,Uganda na Burundi tayari wameshawasili nchini na jana wameelekea wako mkoani Morogoro kushiriki shughuli za kijamii.
Mratibu wa onyesho hilo, Ally Masoud Kipanya amesema hili ni kundi la tatu kushiriki shughuli za kijamii, ambapo kundi la kwanza lilikuwa Iringa, kisha la pili likaenda Zanzibar na hili la tatu linaenda Morogoro kushiriki shughuli za kijamii, huku lengo kubwa likiwa ni kubadilisha maisha ya wanajamii wa huko.
“Hii ndio sababu Maisha Plus ya mwaka huu inaitwa Maisha Plus Rekebisha, ambapo lengo kuu ni kuangalia matatizo ya eneo husika na kuangalia jinsi ya kutatua, na sio kulalamika, tunataka kurekebisha wananchi wenye fikra za kusubiri kufanyiwa, kuwa wepesi wa maamuzi na kutatua matatizo waliyonayo”, alisema Masoud
“Wananchi wengi hulalamikia serikali juu ya maswala mbalimbali ambayo hata wao wenyewe wanaweza kuyarekebisha bila kusubiri kufanyiwa”,alisema.
Washiriki kutoka nchi jirani ni walio mkoani Morogoro kwa sasa ni Loveness Asantely ,Mary Sidi(kutoka Kenya), Borandanginye Aurore, Mvano Ciza, na Abdou Karim(kutoka Burundi), Aminata Siira(kutoka Uganda), Uwamahoro Fatima, Ngabozinza Khalid, na Ngabozinza Daniel (kutoka Rwanda)
Kupitia Maisha Plus Rekebisha mwaka huu, wananchi watapata elimu juu ya kuepukana na mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo magonjwa kama malaria, kipindupindu, homa ya manjano na mengineyo.
Washiriki wote kwa ujumla kutoka nchi za jirani wanatakiwa kuwa 12 nambili,waliofika nchini ni 10 wawili wanaotambulika kwa majina Said Rashid (Uganda) na Caron Abisai (Kenya) bado hawajafika.
 
Previous
Next Post »