Sababu za kupotea kwake;
Ukiongelea jina kama Z-anton kwa wengi watakuwa wanamjua msanii huyu maarufu kwa wimbo wake uitwao binti kiziwi,unaweza kusema kuwa ni moja ya waasisi wa muziki huu wa bongo fleva, ambao wameweza kukusanya wapenzi wengi wa muziki huu wa bongo fleva,nakuweka mchango mkubwa katika kukuza muziki huu na kufanya uweze kupendwa na mashabiki wa kila rika…na kama ulikuwa unajiuliza huyu mtu yuko wapi,.. he is back! anakuja tena na nguvu mpya hivi sasa katika game hili la muziki wa bongo fleva.
Akiwa anahojiwa na kipindi kimoja cha television nchini Kenya amefunguka nakusema kuwa upotevu wake katika game la muziki huu,ni kutokana na matatizo ya hapa na pale yakifamilia na kibinafsi zaidi aliyokuwa anakabiliana nayo,ila kwa hivi sasa its all gud,yuko teyari kurudi kwenye game.
Kuhusu muziki wake;
Kuhusu muziki anafunguka na kusema kwa sasa amerudi katika game na nguvu mpya kabisa,ingawa kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wanamwekea vizingiti ili asiweze kurudi katika game hili la bongo fleva,ila kwa hivi sasa anarudi kipekee zaidi,hii yote ni baada ya kujitoa katika kundi lake la zamani la tiptop connection na kuongezea kuwa hana mpango hata wakurudi kundini cause anataka kufanya masuala yake ya muziki mwenyewe,bila ya kutegemea mkono wa mtu yeyote Yule kwa hivi sasa.
Maisha yake ya mahusiano baada ya binti kiziwi kukamatwa;
Rumors zilikuwa za kweli kwamba mpenzi wake aliyekuwa amekamatwa huko nchini china amefungwa kutokana na kosa la kuingiza madawa ya kulevya,na zaidi ni kuwa huko aliko anatumikia kifungo cha miaka sita,ila kwa upande wa Z-anton, hayo yote hayamhusu kwa sasa ,cause walishatemana siku nyingi na habari ya mujini ni kwamba hivi sasa anampenzi mwingine ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.
CREDIT:UDAKU MAGAZINE
EmoticonEmoticon