KIM KARDASHIAN ANUSURIKA KIFOBAADA YA KUPATA AJALI YA GARI


Kim Kardashian






























WAKATI akiwa katika maandalizi ya harusi yake mwanamitindo ambaye pia ni mchumba wa msanii wa Hip Hop nchini Marekani Kim Kardashian jana alipata ajali ya gari ambayo haikuwa na madhara makubwa wakati akiendesha gari lake aina ya Mercedes G Wagon na kukwaruzana na Nissan Sentra.

Hata hivyo, gari la Kim Kardashian halikuharibika zaidi mkwaruzo mdogo iliupata lakini Nissan Sentra inadaiwa kuharibika vibaya sehemu ya mbele.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia TMZ kuwa Kim Kardashian alikuwa anakata kona kuelekea kushoto wakati dereva wa gari aina ya Nissan alikuwa anaonesha ishara ya kuelekea kulia, lakini kwa bahati mbaya badala ya kulekea kulia alinyooka na barabara na kulifikia gari la Kim K na kusababisha magari hayo kukwaruzana.

Imeelezwa kuwa wawili hao waliendesha hadi Beverly Hills Hotel ambapo walizungumza na kuyamaliza na kila mmoja akaendelea na safari yake bila polisi kuhusika.
Previous
Next Post »