Shangazi wa Kenyatta atekwa na kuibiwa Nairobi

Uhuru Kenyatta mgombea kiti kwa niaba ya chama tawala KANU akizungumza na Wakenya wa Ulaya Disemba 2002

Shangazi wa Rais Uhuru Kenyatta amekuwa moja wapo wa waathiriwa wa wizi wa magari kwa kutumia nguvu nchini Kenya, baada ya kushambuliwa na kuibiwa gari lake akiwa katika msongamano wa magari kwenye njia kuu ya Uhuru.

Watu watatu walokuwa na bunduki walingia kwa nguvu ndani ya gari la Bi. Njeri Muhoho, mwenye umri wa miaka 56, na kumzungusha katika jiji la Nairobi kwa karibu saa mbili kabla ya kumshusha karibu na shule moja ya kimataifa katika mtaa wa kaskazini wa Gigiri.

Bi. Muhoho, ambae ni mke wa mkuu wa zaamani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya, George Muhoho, aliwambia polisi kwamba alikua garini pamoja na mwanamume mwenye umri wa miaka 25 wakati gengi la watu watatu walipowashambulia Jumanne, saa mbili na nusu usiku.

Polisi wanaeleza kwamba walishambuliwa wakiwa wanasubiri taa ya kuongoza magari kubadilika kuwa kijani, na aliibiwa Sh 20,000 za Kenya, pamoja na kadi yake ya benki ATM, na leseni ya kuendesha gari.

Mkuu wa polisi mjini Nairobi Benson Kibue anasema baada ya kuwashusha, wezi hao watatu walelekea mahala isipojulikana na gari lao la aina ya Nissan. Msako unafanyika kutafuta gengi la watu hao.


SOURCE:VOA
Previous
Next Post »