TAARIFA KUHUSU MCHEZO KATI YA MBEYA CITY FC NA RHINO RENGERS 8/3/2014


Ndugu naomba kutumia nafasi hii kutoa taarifa kuwa Mbeya City Fc hatukufurahishwa na aina ya mchezo wa kibabe ulioonyeshwa na wachezaji wa club ya Rhino Rengers katika mechi iliyochezwa jana jumamosi 8/3/2014 katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Mbeya.

 
Nasema hivyo kutokana na mchezo mbaya uliosababisha wachezaji wetu Richard peter na Mwigane Yeya kuumizwa vibaya kwa makusudi,Rechard aliumizwa vibaya na mlinda mlango wa Rihno baada ya kumrukia kwa miguu yote miwili hivyo kusababisha madhara makubwa katika mbavu zake za kushoto, mchezaji huyu yuko kambini anaendelea na tiba chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari kutoka hospitali ya rufaa Mbeya pamoja na daktari wetu wa timu.

Na kwa upande wake mwigane yeya aliumizwa vibaya na huyohuyo mlinda mlango wa Rihno baada ya kumrukia vibaya na kumkwaruza vidole macho yote mawili hivyo kumfanya mchezaji wetu kushindwa kuona kabisa na anaendelea na matibabu chini ya doctor wetu.

Pamoja na hayo hatukufurahishwa kabisa na nidhamu iliyoonyeshwa na mwalimu msaidizi wa club hiyo ambae katika mchezo mzima alikuwa akitamka maneno yasiyo na staha tofauti na mchezo wa mpira wa miguu unavyoelekeza, na kwa kudhihirisha hilo baada ya mwalimu huyo kutelewa kwenye benchi na mwamuzi alisikika akiwahamasisha wachezaji wake kuwaumiza wachezaji wetu kwa kusema “wagongeni tu hao” na ndicho kilichotokea

Kwa maana hiyo basi kwa niaba ya club tumeumizwa sana na aina isiyofaa ya uchezaji waliounyesha wachezaji wa Rihno Rangers na pia tunasikitika sana kuona aina hii ya uchezaji unaendelea kufumbiwa macho sisi Mbeya City Fc tunaamini nidhamu ndio ushindi.
Pamoja na yote tunaomba mamlaka zote zinazohusika na VPL zikiongozwa na TFF waitazame upya mechi hiyo ili kulinda nidhamu ya ligi kuu na kutoa maamuzi sahihi.
 
 
 
Ndugu mwana habari naomba pia kuweka sawa mkanganyiko uliojitokeza jana kuhusu mfungaji wa goli la kwanza goli hilo lilifungwa na Paul Nonga na si saady kipanga kama ambavyo vyombo vingi vya habari vililiripoti.

ASANTENI

FREDDY JACKSON 
Afisa habari MCC FC
Previous
Next Post »