TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 11.03.2014.
· MAGARI MATATU YAGONGANA NA KUSABABISHA KIFO CHA
MTU MMOJA NA MAJERUHI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WANAWAKE WAWILI KWA TUHUMA ZA WIZI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
MWANAMKE MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MAGARI MATATU YAGONGANA NA KUSABABISHA
KIFO CHA MTU MMOJA NA MAJERUHI.
GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.156 AZF
AINA YA TOYOTA CRESTA LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ALEX MBWAGA (22) MKAZI WA KABWE LILIGONGA KWA NYUMA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.746 CME
AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ANDREW JOHN (40) MKAZI WA UYOLE NA KISHA KUGONGA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.925 BQW
AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FELEX MWAKALINGA (32)
MKAZI WA SOWETO NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA WA GARI T.156 AZF AINA YA TOYOTA CRESTA. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA 05:45HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA
MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA
IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA
BARABARA YA MBEYA/NJOMBE. AIDHA KATIKA AJALI HIYO STELA VASCO (22) MKAZI WA SOWETO NA LEONARD TITO (21) MKAZI WA KABWE WALIOKUWA KWENYE GARI T.156 AZF TOYOTA CRESTA WALIPATA
MAJERAHA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI WA GARI T.156 AZF. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WANAWAKE WAWILI KWA
TUHUMA ZA WIZI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WANAWAKE WAWILI [02] KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUHUMA ZA
WIZI AMBAO NI 1.RUKIA RASHID [24] NA 2. JAMIRA ABDALAH [38] WOTE WAKAZI WA
TUNDUMA WILAYA YA MOMBA. WATUHUMIWA HAO WALIINGIA KWENYE DUKA LA MFANYABIASHARA
JANETH SIVANUS [28] WAKIWA WAMEVALIA
NGUO MUUNDO WA HIJABU NA KUIBA VITAMBAA VYA SUTI AINA YA POLISTER
MAJOLA NANE [08] YENYE THAMANI YA TSHS 2,400,000/=. KABLA YA TUKIO HILO WATUHUMIWA HAO WALIANZA KUULIZIA
BEI YA BIDHAA HIZO NA KISHA MTUHUMIWA
MMOJA ALIENDELEA KUMSEMESHA MUUZAJI WA DUKA AMBAYE ALIKUWA AKIENDELEA KUHUDUMIA
WATEJA WENGINE WAKATI MTUHUMIWA WA PILI AKITEKELEZA TUKIO LA WIZI. TUKIO HILO
LIMETOKEA TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:50HRS JIONI ENEO LA MWANJELWA KATA YA MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJINI MBEYA. AIDHA MARA BAADA YA KUIBA VITAMBAA HIVYO NA KUONDOKA PASIPO
MWENYE DUKA KUJUA, MAJIRANI WALIMJULISHA
MWENYE DUKA JUU YA TUKIO HILO, JITIHADA
ZILIFANYIKA ZA KUWAFUATILIA WATUHUMIWA HAO NA WALIKAMATWA KARIBU NA GUEST YA
MFIKEMO MTAA WA JUA KALI WAKIWA NA VITAMBAA HIVYO VYA SUTI HIVYO
WALIRUDISHWA KATIKA DUKA HILO. KUFUATIA TUKIO HILO LILIJITOKEZA KUNDI LA
WANANCHI WALIOTAKA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKIWA NA SILAHA ZA JADI
MAWE,FIMBO NA MARUNGU WENGINE WAKIWA NA MADUMU YA MAFUTA AINA YA PETROLI WALIFIKA ENEO HILO KWA NIA YA KUWAPIGA KISHA KUWACHOMA MOTO WATUHUMIWA HAO HATA HIVYO MWENYE DUKA JANETH SIVANUS ALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA HALI HIYO HIVYO
ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIFIKA ENEO HILO ILI KURUDISHA AMANI IKIWA NI
PAMOJA NA KUWAOKOA WATUHUMIWA. KATIKA JITIHADA HIZO JESHI LA POLISI
LILILAZIMIKA KUTUMIA RISASI KWA KUFYATUA RISASI TANO [05] HEWANI ILI
KUWATAWANYA WATU WALIOKUWA WAMEZINGIRA DUKA HILO NA KUFANIKIWA KUWAOKOA
WATUHUMIWA HAO HIVYO KUWAFIKISHA SALAMA KITUO CHA POLISI KATI WAKIWA NA MALI
WALIYOIBA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI SIO TABIA
NZURI NA NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAHAKIKISHE
WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA MTU/WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA
JAMII KUACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA
KWA KUTUMIA NJIA ZA MKATO, KWANI HUWEZI KUPAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO KWA
NJIA ZA MKATO BADALA YAKE WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI KWA LENGO LA KUPATA
KIPATO HALALI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ANASTAZIA
KATIMA (32) MKAZI WA MAKONGOLOSI
WILAYA YA CHUNYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO
[05]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIPEMBAWE
WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI
WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO].
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
EMANUEL AGUSTINO (24) NA 2. JILALA
GWISU (25) WOTE WAKAZI WA KIJIJI
CHA SAZA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA MTAMBO MMOJA
WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]. WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYWA MNAMO TAREHE 10.03.2014
MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZIFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA KALI ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon