Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Mathayo Torongey kuwa mgombea rasmi wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze.



Mgombea Ubunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chadema, Mathayo Torongey akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana baada ya kutambulishwa. 

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Mathayo 
Torongey kuwa mgombea rasmi wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze.

Akimtambulisha mgombea huyo kwa Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema alisema Torongey alipitishwa juzi na Sekretariati ya chama kwa niaba ya kamati kuu.
“Kikao cha Sekretariati kilizingatia maoni na ushauri wa wanachama na viongozi wetu wa ngazi za chini, Hivyo kwa kuwa hakukuwa na kipingamizi chochote juu ya agombea, chama kilimpitisha Torongey” alisema Mrema
Previous
Next Post »