TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.03.2014.
Ø JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA MAKOSA
MBALIMBALI KUTOKANA NA MISAKO
ILIYOFANYIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WATANO [05] KWA TUHUMA
ZA MAKOSA MBALIMBALI KUTOKANA NA MISAKO ILIYOFANYIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WATANO [05] KUHUSIANA NA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI. KATIKA TUKIO LA KWANZA ALPHONCE PATRICK [19] MKAZI WA KIJIJI
CHA MBALA WILAYA YA CHUNYA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE 10 ZENYE UZITO WA GRAM
50. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 11.03.2014
MAJIRA YA SAA 15:13 ALASIRI KATIKA
KIJIJI CHA MBALA, KATA YA MBALA, TARAFA YA KWIMBA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
AIDHA WATU WENGINE WAWILI 1.KILLY SHUSHA [18]
NA 2. MLAWA SAKSON [18] WOTE WAKAZI
WA KIJIJI CHA MAGAMBA WILAYA YA CHUNYA WALIKAMATWA NA JESHI LA POLISI
WAKIWA NA BHANGI GRAM KUMI [10]. TUKIO
AMBALO LILITOKEA TAREHE 12.03.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA
KIJIJI NA KATA YA MAGAMBA, TARAFA YA SONGWE, KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA
JESHI LA POLISI.
KATIKA TUKIO JINGINE WATU WAWILI 1. CHAZALI
INYAMAGOHA [45] NA 2. SAMWEL MTOKOMA [50] WOTE WAKAZI WA
KIJIJI CHA ISONGOLE WILAYA YA ILEJE WALIKAMATWA WAKIWA NA MALI
IDHANIWAYO KUWA YA WIZI. CHAZALI INYAMAGOHA ALIKAMATWA AKIWA NA MIFUKO MINNE [04] YA SIMENTI NA SAMWEL MTOKOMA ALIKAMATWA AKIWA NA NONDO 55 MALI INAYODHANIWA KUWA NI YA WIZI KUTOKA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.03.2014
MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA
KIJIJI HICHO CHA ISONGOLE TARAFA YA BULAMBYA, KUFUATIA DORIA /MSAKO
ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUACHA
TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA KUTUMIA
NJIA ZA MKATO KWANI HUWEZI KUPAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO KWA NJIA ZA MKATO
BADALA YAKE WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI KWA LENGO LA KUPATA KIPATO HALALI
IKIWA NI PAMOJA NA KUNUNUA MALI HALALI KATIKA SEHEMU HUSIKA. PIA KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI NA
KWA WAKATI KUHUSIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon