Tatizo la kuwepo kwa maji taka na mapipa ya taka karibu na maeneo ya kutayarishia vyakula,ni taswira ya kawaida kwenye vitongoji duni. Hali hiyo hupelekea wakaazi kupatwa na magonjwa kama vile ya kuendesha na hata kipindupindu. Lakini wanawake katika mtaa wa mabanda wa Mathare wamejitolea kukabiliana na matatizo hayo,kwa kutumia teknolojia ya kibofu, au baloon. Mwanahabari wetu alishuhudia jinsi wanawake hawa wanavyotekeleza shughuli hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo. .
EmoticonEmoticon