SIMULIZI TAMU YA WEMA SEPETU

Mwandishi: Imelda Mtema
WEMA Isaac Abraham Sepetu si jina geni Bongo, ni suptastaa aliyetokana na kushiriki mashindano ya  kugombea Taji la Miss Tanzania 2006,  akashinda. Pia anafanya vizuri kwenye filamu za Kibongo.
Ni mrembo mwenye historia ndefu ikisindikizwa na matukio mabaya na mazuri katika kipindi chote tangu ashike taji hilo mpaka sasa.
Wema Sepetu alipotwaa taji la Miss Tanzania 2006.
Katika mahojiano na Amani mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema ambaye ni mtoto wa mwisho wa aliyewahi kuwa waziri wa kwanza wa habari na utangazaji wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoungana na Chama cha Afro Shirazi (ASP), alianika maisha yake ‘ei tu zedi’ kama ifuatavyo:
Amani: Kwa kuanza Wema, tuambie mko wangapi katika familia yenu ya marehemu mzee Sepetu.
Wema: (huku akiachia tabasamu) tupo wengi kidogo, wanne.  Wa kwanza yupo Marekani anafanya kazi, wa pili yupo hapa Bongo, ameolewa. Wa tatu pia yupo  Marekani anasoma na anafanya kazi, mimi ni last born (mtoto wa mwisho).
Amani: Hivi, ulijiandaa kuwa Miss Tanzania mwaka 2006?
Wema: (kicheko) sikujiandaa. Kwanza nilikuwa naiona ipoipo tu. Sikuwahi kufikiria kabisa.
Wema akiwa na mama yake pamoja na marehemu baba yake enzi za uhai wake.
KUMBE MZEE SEPETU NDIYO CHANZO
Wema aliendelea kusema kuwa, baba yake mzazi marehemu mzee  Sepetu ndiye alikuwa chachu ya yeye kujitumbukiza kwenye mashindano ya urembo nchini.
“Baba yangu mzee Sepetu, Mungu amrehemu alipo, alikuwa akiyapenda sana Mashindano ya Miss Tanzania, kila mwaka alikuwa anashiriki kushuhudia tena kwa kukata tiketi mapema.
“Nakumbuka mwaka 2003, ule wa Sylvia (Bahame) tulikuwa nyumbani tukiangalia mashindano kwa runinga kwa sababu baba alikosa tiketi siku hiyo, akasema kumbe kuangalia mashindano kwenye runinga nyumbani ni vizuri sana, akasema anatamani siku moja amwone binti yake mmoja anashiriki hata kama hatashinda.
“Lengo lake lilikuwa akate tiketi akijua anayekwenda kumwangalia ni binti yake. Hata hivyo, sikuhifadhi akilini neno lake. Baada ya kushiriki 2006 na kutwaa taji ndipo nilipokumbuka maneno yale, siku moja tukiwa sebuleni nikamuuliza kama anakumbuka kauli yake, akasema anaikumbuka vizuri.”
Wema Sepetu.
ANAYAONAJE MAISHA BAADA YA KUWA STAA
“Kwanza nianze kwa kusema kwamba nilishajuta sana kuwa staa, lakini ikafika mahali Mungu ndiyo kanipangia kuwa hivi, kwa hiyo majuto yanatokea kwa kila mtu.
“Ila ninachomshukuru Mungu ni kwamba, mpaka sasa nina marafiki wengi ambao nilikuwa nao kabla sijawa miss na baada ya kuwa lakini hatuna mazungumzo ya ndani sana.
“Unajua baada ya kuwa miss nilikutana na watu wapya kikazi. Pia ujue niliingia kwenye filamu, kwa hiyo  nilikutana na wapya wengine.
Ray C.
KUMBE K-LYNN, RAY C WALIKUWA WAKIMZINGUA
Amani: Kabla ya kuwa staa, naamini kuna mastaa waliokuwa wakikuvutia, ni akina nani hao Wema?
Wema: (anatabasamu) kama angetokea mtu na kuniuliza napenda kuwa kama nani, ningemjibu nataka kuwa air hostess (mhudumu kwenye ndege). Kwa  sababu dreams (ndoto) zangu zilikuwa huko.
Ila watu waliokuwa wakinivutia nikiwaona miaka ile ni Ray C (Rehema Chalamila) na K-Lynn (Jacqueline Ntuyabaliwe).
Jacqueline Ntuyabaliwe.
“Nakumbuka tulikuwa tukitoka shule na wenzangu tunakwenda kwenye duka la Mpemba mmoja kula sambusa, sasa magari yaliyokuwa yakipita nilikuwa namuona Ray C au K-Lynn.
“Ila nilikuwa naona wananizingua na umaarufu wao kwa sababu mimi Wema sikuwa na ndoto za kuwa maarufu.”
Wema.
NI LINI ALIANZA MAPENZI?
Wema: (akionesha umakini) nilianza mapenzi mwaka 2005 wakati nashiriki Miss Dar Indian Ocean, ingawa mpenzi wangu huyo  simtaji jina. Huyu sweet niliachana naye baada ya kushiriki urembo mwaka huo.
“Awali aliniambia nikishiriki mashindano ya urembo mimi na yeye basi, yaani hakupenda, alijua nitakuwa mtu wa watu wengi.
“Hata hivyo, nilishiriki kwa siri na siku ya shindano nilishtuka kumuona akiwa mbele anapiga picha. Lakini alinielewa kwani aliendelea na mimi mpaka nilipofika Miss Tanzania, baada ya hapo, kwa sababu nilikuwa bize sana nikawa sionani naye, kila akinipigia simu nipo bize, yeye mwenyewe akasema tuachane, tukaachana lakini hadi sasa tunasalimiana vizuri tu.”
Wema akiwa na marehemu Kanumba.
MARA YA KWANZA KUKUTANA NA KANUMBA WALIKISI MARA MBILI
Amani: Vipi kuhusu Kanumba?
Wema: (anaonesha masikitiko) siku ya kwanza kukutana na Kanumba, da! Mungu ailaze mahali pema roho yake. Nilikuwa na dada yangu anayeishi Sinza, maana nilikuwa naishi kwake. Siku hiyo mimi na dada tulikuwa mitaani tukitafuta carpet (zulia).
“Tulifika nje ya duka moja tukamkuta Kanumba na makamera yao ya muvi pale. Akatokea Mayasa Mrisho (Maya) tukasalimiana, akaniambia amenipenda sana, nikamjibu mimi pia, tena napenda anavyoigiza.
“Akapaza sauti kumwambia Kanumba umemuona Wema, Kanumba akasema ooo, sawa nimemuona, lakini akaendelea na shughuli zake. Aliniringia f’lani hivi.

SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS
Previous
Next Post »