TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 25.03.2014.
·
BASI LA ABIRIA
MALI YA KAMPUNI YA MABASI YA HOOD
LIMEACHA NJIA NA KUPINDUKA.
·
WATU WAWILI WAFARIKI
DUNIA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI ZA
BARABARANI WILAYA YA MBEYA MJINI NA RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA BAADA
YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO].
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
BASI LA ABIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.751 AVL AINA YA SCANIA MALI YA
KAMPUNI YA MABASI YA HOOD LINALOFANYA SAFARI ZAKE ZA DAR – KYELA LIKIWA
LINATOKA KYELA – MBEYA KUELEKEA DAR LIMEACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA ENEO LA
INYALA MKOA WA MBEYA.
BASI HILO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA FIDELIST MBUYA (55)
MKAZI WA MKOANI PWANI. AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA 07:30 ASUBUHI YA LEO
KATIKA ENEO HILO LA INYALA. CHANZO CHA AJALI HIYO INADAIWA NI MWENDO KASI WA
BASI BAADA YA DEREVA WAKE KUSHINDWA KULIMUDU WAKATI MBELE YAKE KULIKUWA NA GARI
DOGO LA ABIRIA AINA YA TOYOTA HIACE ILIYOKUWA INATAKA KUTEREMSHA ABIRIA HALI
ILIYOPELEKEA KWENDA PEMBENI YA BARABARA UPANDE WA KUSHOTO NA KUPINDUKA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO ABIRIA WAPATAO WATANO
WAMEJERUHIWA NA WANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA,
HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. DEREVA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA BARABARNI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
MATUKIO MAWILI YA AJALI ZA BARABARANI:
MTU MMOJA MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA
LA GWASA
MWENYE UMRI KATI YA
MIAKA 20-25 ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.493 AGF/T.213 BMA AINA YA
SCANIA LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ERASTO
MNDENDEMI [34] MKAZI WA IFISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 24.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:30
ASUBUHI ENEO LA IYUNGA, KATA NA
TARAFA YA IYUNGA BARABARA KUU YA
MBEYA /TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI HIYO
NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU
ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
AIDHA KATIKA TUKIO LA PILI, MTU MMOJA [MZEE] MTEMBEA KWA MIGUU STWELILE KIBONA [70]
ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI
YA MAKANDANA – TUKUYU WILAYA YA RUNGWE BAADA YA
KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 24.03.2014 MAJIRA YA SAA
20:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA
LUGOMBO, KATA YA ILIMA, TARAFA YA PAKATI
BARABARA KUU YA MBEYA /TUKUYU. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
HIYO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARNI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI
WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA
MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING]
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA
NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
KATIKA
TUKIO JINGINE:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NERE MWALEMBESI [55] MKAZI WA MWANJELWA
JIJINI MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05] .
MTU HUYO ALIKAMATWA TAREHE 24.03.2014 MAJIRA YA SAA
11:00 ASUBUHI ENEO HILO KUFUATIA
MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA. MTUHUMIWA HUYO NI
MTENGENEZAJI/ MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon