Lupita Nyong’o, muigizaji wa kike toka Kenya anaendelea kung’aa na kuwa mada
ya kuzungumziwa
hata na watu maarufu na sasa amemkuna kichwa rapper mkongwe Jay Z na ameamua
kumuweka
Kushinda tuzo kubwa ya Oscar kupitia filamu ya 12 Years A Slave ni kitu ambacho
kimeyabadilisha
kabisa maisha ya mrembo huyu na kumuweka rasmi kwenye orodha ya watu
maarufu zaidi
kwenye kiwanda cha filamu duniani kwa mwaka 2013/2014.
Jay Z amemtaja
Lupita Nyong’o kwa kumpa sifa yeye na filamu ya 12 Years A Slave
kwenye wimbo
alioshirikishwa na Jay Electronica akiwa amefanya kama mtindo huru, wimbo unaitwa
‘We Made It’.
“I’m om my Lupita Nyong’o/ Stuntin on stage after 12 Years A Slave
This Ace of Spades look like an Oscar /Black tux, look like a mobster. Amerap Jay Z.
Kuna uwezekano kabisa kuwa Beyonce na Jay Z waliwahi kumzungumzia Lupita kwa
mazuri kama
wanafamili na ndio maana alimuingia akilini wakati anachora mistari hiyo.
Well, huenda tukasikia siku moja rais Obama ambaye ni rafiki mkubwa wa
Jay Z akimtaja
Lupita Nyong’o kwa mazuri.
Jay Z pia alimtaja Drake kwenye wimbo huo na kujibu kile ambacho Drake alikisema
kuwa siku hizi
Jay Z hawezi kurap bila kutaja angalau baadhi ya vitu vya sanaa ya rap (michoro n.k)
wakati
anazungumzia jinsi anavyopenda sanaa ya michoro.
Jay Z alieleza kuwa siku hizi kuna watu wanarap kuhusu vitu ambavyo hawafanyi tofauti na yeye anayerap kile anacho fanya.
“Sorry Mr. Drizzy for so much art talk/ Silly me, rappin’ ’bout sh-t that I really bought
While these rappers rap about guns that they ain’t shot/ And a bunch of other
silly sh-t that
they ain’t got.”
Usikilize hapa wimbo wa Jay Electrica ‘We Made It’:
EmoticonEmoticon