TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 21.02.2014.








·         MPANDA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KOSA LA KUJERUHI.


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA WATANO  WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI NA ZILIZOISHA MUDA WAKE.

 MPANDA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.


MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BONIPHACE MWALUM (43) MWENDESHA PIKIPIKI, MKAZI WA ILONGO WILAYA YA MBARALI ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI IT 5239 AINA YA TOYOTA CALDINA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMIRI MUGASA (44) MKAZI WA TABATA JIJINI DAR-ES-SALAAM. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI, DEREVA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI YAKE. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA UASALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU YENYE VIVUKO YAANI ZEBRA CROSSING ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.



JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KOSA LA KUJERUHI.


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEOFREY EDSON (16) MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA BAADA YA KUMJERUHI KWA KUMCHOMA KISU TUMBONI JASTINE ASAJILE (19) MKAZI WA MAKUNGULU. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE. CHANZO NI UGOMVI ULIOTOKEA BAINA YAO WAKIWA WAMELEWA POMBE KWENYE KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KIITWACHO MBAGA. MHANGA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI YAKE. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO. PIA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTEMBEA NA SILAHA KATIKA SEHEMU ZA STAREHE KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.






  
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA WATANO  WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI NA ZILIZOISHA MUDA WAKE.


KATIKA OPERESHENI INAYOENDESHWA NA JESHI LA POLISI  MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA [TFDA] MKOA WA MBEYA, JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA WATANO 1. JENIPHER SANGA (25) MKAZI WA SOWETO, 2.SHUKURANI AMBILIKILE (18) MKAZI WA IYUNGA, 3. ASWILE ASUKILE (31) MKAZI WA AIRPORT, 4. MEGU AMOS (28) MKAZI WA IYUNGA NA 5. OSEAH JOHO (32) MKAZI WA ISANGA WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI NA ZILIZOISHA MUDA WAKE WA MATUMIZI. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA WAKIWA NA POMBE KALI KONYAGI CHUPA NDOGO 48, KONYAGI CHUPA KUBWA 04, KONYAGI VIROBA BOKSI 66 NA POMBE KALI AINA YA VALUE CHUPA 23. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. PIA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WAKE WA MATUMIZI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WANAO JISHUGHULISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA ZILIZOISHA MUDA WAKE AZITOE KWA JESHI LA POLISI AU KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.




SIGNED BY:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »