Soulja Boy atangaza kuwa atafungwa jela wiki hii


Katika hali ambayo haikutugemewa, rapper Deandre Cortez Way aka Soulja Boy amewaambia mashabiki wake kuwa ataenda jela.
Rapper huyo mzaliwa wa Chicago ametweet February 15 na kuonesha kuwa baada ya siku tano ataenda jela. Hii ina maana itakuwa wiki hii mwishoni.
“5 more days until I go to jail. Appreciate everyone who was there for me while I needed y'all.” Alitweet Souja Boy bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Lakini mwishoni wa mwezi uliopita  iliripotiwa kuwa rapper huyo alishitakiwa kwa kosa la kuwa na bunduki na kuvuka bila kusimama katika eneo alilopaswa kusimama huko Los Angeles.
Previous
Next Post »