Mke wa 2Face Idibia, Annie Idibia ameshindwa kuvumilia baada ya kusoma habari iliyoandikwa na jarida la ‘Icon’ la nchini humo kuwa mume wake amempa ujauzito mfanyakazi wa Bank aliyetajwa kwa jina la Teniola.
Annie ametweet akiuponda mtandao ulioandika habari hiyo kwa kunukuu kile kilichoandikwa na jarida la Icon, na kudai kuwa na wao hawana utofauti na jarida hilo aliloliita ‘jarida bubu’.
“@AfricanCelebSpy hope u have gotn al d traffic needed 4 ur blog?Thr’s no diff b/w u n dumb icon mag!Evil ple tryn 2 take d suga out of our tea.” Alitweet Annie.
Jarida la Icon liliandika habari kuwa 2face alikuwa na uhusiano wa mapenzi kwa muda mrefu na mfanyakazi huyo wa bank na kwamba tayari ana ujauzito wa miezi mitatu wa mwimbaji huyo wa Naija.
Liliongeza kuwa chanzo chao kimesema mwimbaji huyo ameshambembeleza mfanyakazi huyo autoe ujauzito huo huku akimuahidi kumpa gari mpya endapo atafanya hivyo.
EmoticonEmoticon