JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
RPC. Ofisi ya Kamanda wa
Polisi,
Mkoa wa Mbeya, Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
E-mail:-
rpc.mbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 20.01.2014.
WILAYA YA MBARALI –
MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 19.01.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA
YA ITAMBOLEO, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI NA MKOA WA MBEYA,
MTOTO LUMIKI S/O RAHIM, MIAKA 06,
MMASAI, MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI KAPUNGA DARASA LA KWANZA ALIUAWA KWA KUPIGWA
NA FIMBO KICHWANI NA MTOTO BEDON S/O
SAID, MIAKA 12, MUWANJI, MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI KAPUNGA DARASA LA SITA.
CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUDUMISHA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO WANGALI
WADOGO ILI WAKUE KATIKA MISINGI NA USTAWI MZURI WA JAMII NA KUJIEPUSHA NA
VITENDO VYA UHALIFU.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon