Kumekuwa na machafuko zaidi katika Jamhuri ya Afrika ya kati, siku moja kabla ya baraza la mpito kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, ameona miili ya Waislamu wawili iliyoteketezwa moto.
Wapiganaji wa Wakristo wamesema waliwaua watu hao kulipiza kisasi mauaji ya awali ya muumini mmoja wa dini ya Kikristo.
Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu, ICRC, inasema machafuko mapya ya kidini yalizuka siku ya Jumapili Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Muungano wa Ulaya unatarajiwa leo kuidhinisha kutumwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Ulaya kujiunga na wale wa Afrika na Ufaransa walio nchini humo.
Mauaji hayo yanasadikiwa kuchochea machafuko mapya mjini Bangui
MAPIGANO YA KIDINI
Mtu wa kwanza aliyeuawa anasemkana kuwa ni Mkristo mmoja aliyejulikana vyema kutoka mtaa unaoitwa Sangoh.
EmoticonEmoticon