MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YATEKETEA KWA MOTO.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA       
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



 



RPC.                                                                                                                                   Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Mkoa wa Mbeya,                                                                                 Namba ya simu 2502572                                                                                                                              S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                                                       MBEYA.
E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                 





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 28.01. 2014.




·         MTU MMOJA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.







·         MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YATEKETEA KWA MOTO.















MTU MMOJA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YONA KAIZA @ SIMKONDA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA YALA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI KWA KUTUMIA SILAHA BUNDUKI AINA YA GOBOLE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITUKEA MNAMO TAREHE 27.01.2014 MAJIRA YA SAA 03:30HRS BAADA YA WATU HAO KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KUPIGA HODI, MAREHEMU ALIPOFUNGUA MLANGO ALIPIGWA RISASI KIFUANI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. HAKUNA KITU KILICHOCHUKULIWA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KWA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YATEKETEA KWA MOTO.

MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YAMETEKETEA KWA MOTO NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI. TUKIO HILO LILILOTOKEA TAREHE 27.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:15HRS HUKO MBALIZI FIDELIS DANIEL (54) MKURUGENZI WA SHULE HIYO ALIGUNDUA KUUNGUA KWA MABWENI MANNE YA SHULE HIYO WANAYOLALA WAVULANA KATI YA MABWENI HAYO MAWILI YAITWAYO STATE HOUSE NA MALCOM X YALITEKETEA KABISA KWA KUUNGUA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA VITANDA 74 WALIVYOKUWA WANALALIA WANAFUNZI NA VITU MBALIMBALI. AIDHA MABWENI YAITWAYO KOFFI ANNAN NA MARCUS YALIUNGUA MOTO AMBAO ULIDHIBITIWA KWA KUZIMWA. JUMLA YA WANAFUNZI 355 WALIKUWA WANAISHI KATIKA MABWENI HAYO. CHANZO CHA AJALI HIYO BADO KUFAHAMIKA KWANI WAKATI TUKIO LINATOKEA WANAFUNZI WALIKUWA MADARASANI. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANAO BAINA YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI, JESHI LA POLISI, WANAFUNZI NA WANANCHI WA ENEO HILO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI ZA MAKUSUDI DHIDI YA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KAMA KUHAKIKISHA KATIKA MAJENGO KUNAKUWA NA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO “FIRE EXTINGUISHER” NDOO ZA KUCHOTEA MCHANGA NA MAJA, KUWEKA MIUNDO MBINU YA BARABARA ZINAZOWEZA KURAHISISHA MAGARI YA KUZIMA MOTO NA UOKOAJI KUFIKA KATIKA MAENEO YA MATUKIO KWA URAHISI.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »