WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI
KUGONGANA NA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 12.12.2013 MAJIRA YA SAA 17:05HRS HUKO MAENEO YA UYOLE BARABARA
YA MBEYA /TUKUYU, KATA YA ITEZI TARAFA YA IYUNGA
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T. 336 ATL AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA HERIEL S/O MZAVA, MIAKA 38, MPARE,
MKAZI WA MOSHI-KILIMANJARO LILIGONGA KWA NYUMA
GARI T.385 BYA AINA YA M/FUSO
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA YONA
S/O MWAKIBENGA, MIAKA 34, KYUSA, MKAZI WA MWANJELWA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HERIEL S/O MZAVA PAPO HAPO. AIDHA KATIKA TUKIO HILO OMARI S/O SALIMINI, MIAKA 22, MPARE,
TINGO WA GARI T.336 ATL M/FUSO,
MKAZI WA MOSHI-KILIMANJARO ALIJERUHIWA
NA KULAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO NI MWENDO KASI WA GARI T.336 ATL. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. PAMOJA NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU
KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI –
TAARIFA YA KIFO.
MNAMO
TAREHE 12/12/2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO MAHANGO KATA YA
MAHANGO TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ZELA D/O MNENWA, MIAKA 2,
MHEHE , MKAZI WA MAHANGO ALIKUFA MAJI KATIKA MTO LYANDEMBELA WAKATI AKIOGELEA
NA WATOTO WENZAKE. CHANZO NI KUZIDIWA NA MAJI HAYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA
UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA
KUNYESHA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUZIBA/KUFUNIKA NA KUFUKIA MASHIMO NA
VISIMA VILIVYOWAZI KWANI NI HATARI KWA USALAMA WA WATOTO.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI–
KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO
TAREHE 12.12.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO MBALIZI KATA YA BONDE LA
USONGWE TARAFA YA USONGWE MBEYA
VIJIJINI. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JIHA S/O LUNYARI, MIAKA 14, MHEHE, MKULIMA NA MKAZI WA SHIGAMBA
AKIWA NA BHANGI KETE 85 SAWA NA UZITO
WA GRAMU
425, MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA
NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. MTUHUMIWA AMEKAMTWA NA TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU
KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMIII HASA VIJANA KUACHA
TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon