WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA
GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 11.12.2013 MAJIRA YA SAA 17:05HRS HUKO MAENEO YA MBALIZI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA
KATA YA BONDE LA SONGWE, TARAFA YA USONGWE,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA
MBEYA. GARI T. 106 ARE AINA YA TOYOTA HAICE LIKIENDESHWA NA DEREVA THOMAS S/O TIBEGIRE, MIAKA 43, MHAYA,
ASKARI WA JWTZ KIKOSI CHA 44 KJ MKAZI
WA MBALIZI LILIGONGANA NA PIKIPIKI STK
4245 AINA YA HONDA IDARA YA KILIMO UYOLE IKIENDESHWA NA JUMA S/O MWASHALA, MIAKA 45, MMALILA, FUNDI MAGARI, MKAZI WA
MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI
TEULE YA IFISI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI NA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA MJINI –
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO
TAREHE 11.12.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO STENDI KUU, KATA YA SISIMBA,
TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA THADELA S/O HARGATHA,
MIAKA 30, RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA ANAKULA CHAKULA KWENYE KIBANDA CHA MAMA LISHE.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU
WANAOWATILIA MASHAKA ILI TARATIBU ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon