Rihanna na Beyonce wampa kigugumizi Jokate Mwegelo, nani adondoke Tanzania kati yao, nani mkali zaidi? Msikilize hapa


Rihanna na Beyonce wampa kigugumizi Jokate Mwegelo, nani adondoke Tanzania kati yao, nani mkali zaidi? Msikilize hapa

Nani mkali zaidi kati ya Beyonce na Rihanna? Hilo ni swali ambalo limezua mjadala kati ya fans wao, lakini nani aje Tanzania mwakani kati ya wawili hao, ni mjadala mwingine mkubwa.
Mrembo, mwanamitindo, mjasiriamali na mtangazaji wa TV Jokate Mwegelo aka Kidoti amepata kigugumizi kumtaja mkali kati ya Beyonce na Rihanna baada ya kupewa nafasi ya kutoa mtazamo wake kupitia ‘The Chart’ ya 100.5 Times Fm.
Mtangazaji wa ‘The Switch’ Raheem Da Prince akiwa na Dj D_Ommy, alimpa assignment Jokate achague mmoja kati ya Rihanna na Beyonce anaependa adondoke Tanzania mwakani, just in case Times Fm wakihitaji kumleta mmoja kati yao.
“Let me te… aah…yaani daah..wote wakali unajua eeh..” Anasikika Jokate aka Kidoti ambaye hivi karibuni alizindua Kidoti Club.
“Yaani kiafrika hivi wote wakati yaani, seriously. Halafu I love both of them for different reasons.” Alifunguka Jokate.
Hata hivyo, ilimbidi azichambue sifa zao wote wawili kwa mtazamo wake.
“Rihanna nyimbo zake zinakick zaidi, but when it comes to presence, vocal...obviously Beyonce takes the crown.” Huyo ni Jokate.
Rihanna alivunja record kwa kufikisha nyimbo 13 kwenye Billboard Chart 200, huku Beyonce akiivunja rekodi ya iTunes kwa album yake mpya aliyoitoa kwa kushitukiza, album iliyopelekea iTunes kuscratch baada ya kuzidiwa na wateja waliotaka kuinunua mapema.
Msikilize hapa:
Source:Times fm
Previous
Next Post »