Rais Dr. Jakaya ametunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa jeshi 208 wa cheo cha Luten Ussu waliohitimu mafunzo yao katika chuo cha mafunzo ya kijeshi TMA kilichoko Monduli mkoani Arusha .
Kabla ya kutunuku kamisheni kwa wahitimu hao wakiwemo 15 waliotoka nchi rafiki Mh rais Dr Jakaya Kikwete ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama alikagua gwaride la wahitimu hao ambalo lilipota mbele yake na kutoa heshima.
Baada ya Mh Rais kutunuku kamisheni kwa wanafunzi hao wa kozi ya 53 ya mwaka mmoja ambao 5 wanatoka Uganda ,4 visiwa vya Shelisheli , 2 kutoka Rwanda na 2 kutoka Swatzaland wanafunzi hao walikula kiapo cha utii kwa Mh rais.
Katika hafla ya kutunuku kamisheni hizo pamoja na kuhudhuriwa na wananchi walikuwepo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo waziri mkuu aliyejiuzulu Mh Edward Lowassa, waziri wa mambo ya ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha, mkuu wa majeshi general Davis Mwamunyange.
Wengine ni pamoja na makamanda wa ngazi mbalimbali za jeshi kutoka ndani na nje ya nchi walioongozwa na general Mirisho Sarakikya, makatibu wakuu walioongozwa na katibu mku kiongozi , pamoja viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa walioongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha bw Magesa Mulongo .
EmoticonEmoticon