Familia ya marehemu Dr. Edimund Sengondo Mvungi pamoja na chama cha NCCR mageuzi, wamewasamehe wale wote waliohusika katika kifo cha Dr. Edmund Sengodo Mvungi na kuwa damu yake inakuwa kafara kwa upatikanaji wa katika bora kwa Watanzania.


Familia ya marehemu Dk Edmund Sengondo Mvungi pamoja na chama cha NCCR-Mageuzi kimewasamehe wale wote waliohusika na kumuua Dkt Mvungi ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba

Rai hiyo imetolewa na msemaji wa familia ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James francis Mbatia wakati wa ibaada maalum ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam

Mbatia amesema Tangu marehemu Dkt Mvungi alipopata tazito la kuvamiwa na watu waliomkata mapanga Novemba 3 mwaka huu hadi mauti yalipompata Novemba 12, yamesemwa maneno mengi, lakini wao kama familia na chama wameamua kuwasamehe wauaji wote

"Tunasema kwamba tumewasamehe, damu ya Dkt Mvungi imeshamwagika, alikuwa mpigania nchiniwe na katiba mpya, sasa amekufa lakini tunafurahi kuona mchakato wa katiba mpya unaendelea na ndiyo ilikuwa dhamira yake"alisema Mbatia

Dkt Mvungi alivamiwa na kukatwa mapanga nyumbani kwake Kibamba jijini dar es salaam hali iliyopelekea kifo chake wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika kusini novemba 12 mwaka huu.
Previous
Next Post »