RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMTEUA DR.ASHA-ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE

DR.ASHA-ROSE MIGIRO ATEULIWA KUWA MBUNGE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.
Previous
Next Post »