USIKUBALI UMASKINI UZEENI

Na Saimeni Mgalula

Maisha ni jinsi unavyo yapangia kuishi maisha ya ovyo au mazuri haya
yote unachagua wewe mwenyewe kuwa tajiri au maskini uchaguzi ni wako.

Ukweli ni kwamba hati ya maisha yako iko mikononi mwako kwa maisha ya
baabae kuitwa tajiri au maskini mwamuzi ni wewe kuishi kwenye nyumba
za kupanga,ujenge nyumba unachagua wewe mwenyewe  kwasababu maisha ni
uchaguzi.

Mwandishi mmoja wa kitabu kiitwacho IT ONLY ME TO CHANGE YOUR LIFE na
mwandishi wake aitwae Will George aliwai kuandika na hapa na mnukuu we
old the key to our distination yani funguo za hatima ya safari yetu ya
maisha ziko mikononi mwetu.

Na kuarika wewe mwenye uchu wa mafanikio maishani twende pamoja na
makala hii kama inavyo jieleza hapo juu.

Leo hii nazungumzia vijana ambao wanaendelea na matendo ya tija huku
hali zao kimaisha zikiwa duni kupita maelezo muda nao ukizidi kuchanja
mbuga.

Katika umri huu ambao kijana ananguvu nyingi na uwezo mkubwa wa
kufikiri na kuchanganua mambo maishani ,anachagua muda mwingi kuwa
bize na mambo ambayo hayana mantiki anapoteza muda bila sababu za
msingi .

Masada anakutana na kijana kwa kumuangalia kila kitu kinajieleza kuwa
hupo duni kimaisha,umri wake unamrusu kufanya kazi kwa nguvu na
kuyabadili kabisa maisha yake lakini cha kushangaza anakuwa busy na
wanawake.

Starehe ni sehemu kubwa ya maisha yake kidogo anacho kipata kinaisha
kwenye pombe  jina lake limetawala kwenye vitabu vingi vya wageni yani
kwenye magesti hii inasikitisha sana.

Hata hivyo jambo moja la muhimu ni kuwa muda huwa refa mzuri wa mchezo
wa wakati wa majuto ukifika muda wenyewe utakukumbusha vyema jinsi
ulivyo upoteza kwa mambo yasiyo na mantikii

Nina eleza hivi kwasababu maisha ni safari ndefu yenye misukosuko
,mabonde ,miba,milima na miinuko ya kutisha,inaitaji watu walio
dhamiria kuyafikia mafanikio maishani kwani njia ya kufika kwenye siku
zote huwa sio nzuri sana.

Mahali popote palipo na utukufu kupafikia njia haiwezi kuwa imenyoka
lakini ukijikaza na kuchukua hatua madhubuti uku ukivumilia tabu na
mateso ipo siku utakula matunda .

Kila binadamu hapa chini ya jua amepewa masaa 24 tu kwa siku,matajili
kama vile Billget ,Waren Bafeti tajiri namba mbili duniani au Karosi
Slim hana zaidi ya masaa 24 kwa siku \tatizo sio masaa 24 kwa siku
tatizo ni jinsi ya kuyatumia,Hapa ndio kwenye daraja kubwa kati ya
tajiri na maskini huu ndo ukuta mrefu unao tenganisha ulimwengu wa
raha na ule wa tabu shida na mateso,

Bahati mbaya sana ni kuwa pamoja na kupewa kiwango sawa cha muda  kwa
siku tunatofautiana jinsi ya kutumia kuna watu hata wakipoteza sekunde
1 ni msiba mkubwa kwao ,lakini wakati huohuo kuna watu hata wakipoteza
masaa 5 au zaidi kwa matendo yasiyo na faida,hai waumizi kichwa hata
siku moja.

Nilikutana na wazee wengi sana ambao wanaishi maisha ya kiudhunisha
mno wanateseka na umaskini wametuama kwenye tope la ufukara lakini 80%
ya wazee hao walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kubadili maisha.

Katika mazunguzo yangu na baadhi yao nilibaki nimepigwa na butwaa
,utakuta mzee bila aibu anasema na hapa nilimnukuu”aaaaaaaa!kijana
mimim nilikuwa na kazi nzuri nilikuwa naishi kwenye zile kota ,sisi
ndio tulio kuwa watumishi wa kutegemewa kwenye zile kampuni lakini
ukimuangalia alivyo kwa sasa machozi yana kulenga lenga kwa huruma
mwisho wa nukuu.

Wote hawa walifanya kosa moja tu maishani mwao huko nyuma kucheza na
muda mambo kufika mwisho na mambo yanapo fika mwisho huwa huwa mwisho
haswaa watati mwingine hutatanisha .

Watu wengi kukubaliana na ukweli pale mambo yanapo fika mwisho hasa
kama walitamani kuona jambo Fulani likiendelea vyovyote vile hata kama
watu na dunia hawata amini ukweli wa mambo kufika mwisho.

Lakini hapa kuna mambo ya kujiuliza ,Ni je umejiandaaje na mwisho wako
pale nguvu ulizo nazo zitakapo fika mwisho upo tayari kikabiliana na
ukweli baada ya uwezo wako mkubwa kufikiria kufika mwisho.

Napenda kutoa angalizo muhimu kuwa achana kabisa na matumizi mabaya ya
muda maishani mwako ujana ulionao kwa sasa ipo siku utafika tamati
kama jinsi kila jambo linavyo fika mwisho.

Nimalizie kwakusema kwamba usikubali kabisa muda uanze kukukumbusha
jinsi ulivyo upoteza wakati huo ukiwa na hali mbaya ya maisha na
tayari ujana ulisha fika mwisho mambo huwa mabaya kuliko neno lenyewe.

MWISHO.
Previous
Next Post »