Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Mboni Show kinachorushwa na kituo EATV Bi Mboni A .Masimba anataraji kula sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na watoto yatima mkoani Iringa .
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,Mboni amesema kuwa akiwa kama mtanzania na mwanahabari ameamua kuandaa chakula cha pamoja na watoto yatima wa vituo vitatu vya mkoa wa Iringa .
Alisema kuwa hafla hiyo ya kula chakula na yatima itafanyika siku ya Desemba 25 mwaka huu ambayo itakuwa ni sikukuu ya Krismas .
Bi Mboni alisema kuwa mbali ya kuendesha vipindi vyake katika kipindi chake cha Mboni Show bado ameguswa kula pamoja na watoto hao 230 pamoja na wageni mbali mbali watakaofikisha idadi ya watu 300.
Alisema kuwa hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Hihglands mjini Iringa na kuwa vituo ambavyo vimealikwa ni pamoja na TOSAMAGANGA , Upendo Centre Sabasaba na YATIMA MOYO KWA MOYO kilichopo Mufindi kata ya Bumilayinga
Hata hivyo alisema mbali ya chakula hicho pia watoto hao yatima watapata zawadi mbali mbali kutoka kwake.
Mboni amesema kuwa amekuwa bega kwa bega na watoto yatima na kuwa mbali ya kula na watoto hao pia amekuwa akifanya hivyo wakati wa sherehe za Ramadhan pia kutokana na kipindi chake kutazamwa na watanzania wote .
Hivyo alisema lengo kuu ni kuwakumbusha watanzania juu ya kuwakumbuka watoto yatima kama ambavyo wamekuwa wakichangia sherehe mbali mbali .
CHANZO :MATUKIO DAIMA
EmoticonEmoticon