MAKALA KWENYE UJASIRIAMALI NG’OMBE WA MASIKINI HUZAA (2)


Katika sehemu ya kwanza ya makala hii, nilielezea  mitazamo mbalimbali na misemo atumiayo binadamu kujikweza au kujishusha,mojawapo ni methali isemayo “Ng’ombe wa masikini hazai” nilieleza kwamba iwapo Ng’ombe wa masikini atatunzwa lazima azae tena naweza kuzaa mapacha. Nilieleza kwa kifupi maendeleo ya ujasiriamali hapa Tanzania na duniani kwa kifupi,aidha niligusia jinsi mataifa ya wenzetu yalivyochukua hatua imara za kumkuza mjasiliamali na ndipo yakatokea mapinduzi ya viwanda.

Wenzetu walitumia mbinu gani mpaka Ng’ombe wa maskini akazaa mapacha? Nitaeleza kwa kirefu hapa chini.

Ikiwa mambo ni magumu,je unayatatua vipi? Moja ya njia ya kuhakikisha kwamba Ng’ombe wetu anazaa ni kujifunza kuwa watafiti na wachunguzi zaidi. Rais Kennedy wa Marekani wa enzi hizo alipata kusema kwamba ukitaka kuendelea katika jamii jiulize malengo yako  ni nini?

Eric Hobsbawm,  katika kitabu chake cha  “How to Change the World: Reflections on Marx and Marxism”anasisitiza kwamba mapinduzi ya viwanda na ujasiriamali 'yalianza' nchini Uingereza katika miaka ya 1780 na hayakuonekana kikamilifu hadi miaka ya 1830 au 1840, ilhali T. S. Ashton anaamini kwamba ilifanyika, kwa kukadiria, kati ya mwaka wa 1760 na 1830. Baadhi ya wanahistoria wa karne ya ishirini kama vile John Clapham na Nicholas Crafts wamedokeza kuwa mchakato wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yalifanyika hatua kwa hatua na kuwa neno mapinduzi halifai kuelezea yaliyofanyika. Hii bado ni mada inayojadiliwa na wanahistoria.


 Mapato ya kiujumla ya Nchi ya kila mtu kwa upana yalikuwa imara kabla ya Mapinduzi ya Viwanda na kuibuka kwa uchumi wa kisasa wa kibepari. Mapinduzi ya viwanda yalianzisha zama za ustawi wa kiuchumi na ulilenga kuleta    mapato ya kila mtu katika nchi zenye uchumi wa kibepari. Wanahistoria wanakubaliana kwamba Mapinduzi ya Viwandani yalikuwa mojawapo ya matukio muhimu sana Kihistoria.
Arnold Toynbee  anayetambulika  kama mwasisi wa  Mapinduzi ya Viwandani, na ambaye hotuba zake zilizotolewa mnamo mwaka wa 1881 zilikuwa na maelezo ya kina. Vyanzo vya Mapinduzi ya Viwandani ni vigumu kuelezea na vinabaki kuwa swala la kujadiliwa, huku baadhi ya wanahistoria wakiamini kuwa Mapinduzi hayo yalikuwa sehemu ya mabadiliko ya kijamii na kitaasisi yaliyosababishwa na kuisha kwa Ubwana nchini Uingereza baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Uingereza katika karne ya 17.
Mapinduzi ya Kilimo ya Uingereza yalifanya uzalishaji wa chakula kuwa rahisi zaidi na kutotegemea wafanyakazi wengi, hivyo kulazimisha idadi ya watu ambao hawengeweza kupata kazi katika kilimo wajiunge na viwanda vya karakana,kwa mfano ushonaji, na baada ya kipindi kirefu wakajiunga na miji na viwanda vilivyokuwa vimejengwa upya wakati huo. Upanuzi wa kikoloni wa karne ya 17 ulioambatana na maendeleo ya biashara ya kimataifa, kuundwa kwa masoko ya kifedha na kukusanywa kwa mtaji pia zinatajwa kama sababu, kama tu mapinduzi ya kisanyansi ya karne ya 17.
Kuwepo kwa soko kubwa la ndani pia unapaswa kutiliwa maanani kama chanzo muhimu cha Mapinduzi ya Viwandani , hasa katika kuelezea mbona yakafanyika nchini Uingereza. Katika mataifa mengine, kama vile Ufaransa, masoko yalipasuliwa na kimkoa, mikoa ambayo mara nyingi ilituza ushuru n a kodi kwa bidhaa zilizouzwa miongoni mwao.
Serikali kuwapa wavumbuzi uwezo wa kipekee wa kuuza ambao ulipimwa chini ya mfumo uliokuwa ukiendelezwa wa patenti ( Katiba ya Uwezo wa Kipekee wa Kuuza 1623) inatambulika kama sababu muhimu.Matokeo ya patenti, mabaya na mazuri, ya maendeleo ya viwanda yanaonyeshwa wazi katika historia ya injini ya mvuke, teknolojia muhimu ya kuwezesha mapinduzi hayo.
Kama malipo ya kuonyesha wazi mbele ya umma jinsi kifaa kilichovumbuliwa kilivyofanya kazi mfumo wa patenti uliwalipa wavumbuzi kama James Watt kwa kuwaruhusu kuwa na uwezo wa kipekee wa kuunda injini za kwanza za mvuke, hivyo basi kuwalipa wavumbuzi na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiteknolojia.
Hata hivyo uwezo wa kipekee wa kuuza kawaida husababisha madhara yanayoweza kuondoa, au hata kuzidi kwa umbali, matokeo mazuri ya kufanya uvumbuzi uwe wazi mbele ya umma na kuwalipa wavumbuzi.
Uwezo wa kipekee wa Watt wa kuunda injini za mvuke huenda kulizuia wavumbuzi wengine, kama vile Richard Trevithick, William Murdoch au Jonathan Hornblower, kuunda injini za mvuke bora zaidi, hivyo basi kuchelewesha maendeleo ya mapinduzi ya viwandani kwa takriban miaka 16.
Baadhi ya wahistoria kama vile David Landes na Max Weber wanaashiria mitazamo mbalimbali nchini Uchina na Ulaya na kuamuru mahali ambapo mapinduzi yalitokea. Dini na imani za Ulaya zilikuwa haswa chanzo cha Ukristo wa Kiyudea, na dhana za Kigiriki. Jamii ya Kichina ilikuwa na msingi wake katika watu kama vile Confucius, Mencius, Han Feizi (Matendo bila Imani), Lao Tzu (Utao), and Buddha (Ubudha).
Watu wa Ulaya walipoamini kuwa ulimwengu ulitawaliwa na sheria za kimantiki na za milele, watu wa Mashariki, waliamini kuwa ulimwengu ulibadilika kila uchao na, kwa Wabudha na Watao, haungeweza kueleweka kimantiki.Kwa sisi Afrika tuliamini kwamba dunia ama ulimwengu ni matokeo ya nguvu inayozidi nguvu zote.
Mjadala kuhusu mwanzo wa Mapinduzi ya Viwanda pia unahusisha jinsi Uingereza ilivyozitangulia inchi zingine na kuzishinda kwa mbali. Kuna watu ambao wamesisitiza umuhimu wa rasilimali za kiasili au za kifedha ambazo Uingereza ilipokea kutoka nchi nyingi za nje ilizozitawala au faida kutokana na biashara ya utumwa ya Uingereza, kati ya Afrika na eneo la Karibiani, iliyosaidia kuendesha uwekezaji wa viwandani.
Imedokezwa kuwa, mbali na hayo, kuwa biashara ya Utumwa na mashamba makubwa ya Uhindi ya Magharibi yalitoa 5% pekee ya mapato ya kitaifa ya Uingereza wakati wa miaka ya Mapinduzi ya Viwandani. Ingawa utumwa ulikuwa chanzo cha faida cha kiasi kidogo cha kiuchumi nchini Uingereza wakati wa Mapinduzi ya Viwandani, mahitaji kutoka eneo la Karibiani yaliambatana na 12% ya pato la viwanda vya Uingereza.
Kwa upande mwingine, biashara kufanywa huru zaidi kutokana na msingi mkubwa wa wabepari huenda ikawa uliruhusu nchi ya Uingereza kutengeneza na kutumia maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia vizuri zaidi kuliko nchi zilizokuwa na milki zenye nguvu zaidi, hasa Uchina na Urusi. Uingereza iliinuka kutoka Vuta vya Kinapolioni kama taifa pekee Ulaya ambalo halikuwa limeharibiwa na utumizi mbaya wa fedha na kuharibika kwa uchumi, na ikiwa meli za kibiashara kubwa za kipekee (Meli za kibiashara za Ulaya zilikuwa zimeharibiwa katika kipindi cha vita na Jeshi la Uingereza la Wanamaji).
Nadharia nyingine ni kuwa Uingereza iliweza kufanikiwa katika Mapinduzi ya Viwandani kwa sababu ya kuwa na rasilimali muhimu. Nchi ya Uingereza Ilikuwa na idadi kubwa ya wakazi katika kila eneo mraba ikilinganishwa na umbo lake ndogo la kijiografia. Kupimwa kwa ardi iliyotumika na kila mtu na mapinduzi ya kilimo yanayohusiana na hili kulisababisha kupatikana kwa wafanyikazi kuwe rahisi.
Hali tulivu ya kisiasa nchini Uingereza tangu miaka ya 1688, na nia zaidi ya jamii ya Kiingereza kukubali mabadiliko (ikilinganishwa na nchi zingine za Ulaya) inaweza pia kusemwa kuwa sababu iliyowezesha Mapinduzi ya Viwandani. Kwa sehemu kubwa, kwa sababu ya Harakati ya Kufungiwa, watu maskini waliangamizwa kama chanzo kubwa cha upinzani dhidi ya kuenea kwa viwanda, na watu wa madaraja ya juu waliendesha maslahi ya biashara yaliyosababisha watu wa kwanza katika kuondoa vikwazo dhidi ya ukuaji wa ubepari (Wazo hili pia limedokezwa katika kitabu cha Hilaire Belloc, Nchi ya Kitumishi.)
Nadharia nyingine ni kwamba mafanikio ya Waingereza yalikuwa kwa sababu ya kuwepo kwa daraja la Kijasiriamali ambalo liliamini kuwa kulikuwa na maendeleo, teknolojia na kazi ngumu. Kuwepo kwa daraja hili mara nyingi huusishwa na maadili ya kazi ya Kiprotestanti (tazama Max Weber) na hasa hadhi ya Wabatizi na madhehebu yanayopingana nao ya Kiprotestanti, kama vile Wakweka na Wapresbiteri ambazo zilikuwa zimenawiri wakati wa Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Uingereza.
Wanahistoria wakati mwingine hutazama kipengele hiki cha kijamii kuwa muhimu sana, pamoja na hali ya uchumi wa mataifa yanayohusika. Ingawa wanachama wa madhehebu haya walitengwa mbali na duru fulani za kiserikali, walitazamwa na Waprotestanti wenzao kama, kwa kiwango kidogo, na wengi katika daraja la kati, wakopaji pesa wa jadi au wanabiashara wengine. Kutokana na kuvumilia huku, kiasi na usambazaji wa mtaji, njia ya kimaumbile ya watu wenye nia ya ujasirimali ya haya madhehebu ingekuwa kutafuta nafasi mpya katika teknolojia zilizoundwa wakati wa mapinduzi ya kisayansi ya karne ya 17.
Kwa mujibu wa muundo wa kijamii, Mapinduzi ya Viwandani yalishuhudia ushindi wa watu wa daraja la kati ya wanaviwanda na wafanyabiashara ambao waliwashinda daraja la watu lenye ardhi ya mabwana wakubwa.
Watu wa kawaida walipata fursa nyingi zaidi za kufanya kazi katika viwanda vipya vya kutengeneza bidhaa, lakini hizi zilikuwa chini ya mazingira magumu ya kikazi yakiwa na masaa marefu ya kazi yaliyotawaliwa na mbio za kufanya kazi za mashine. Hata hivyo, hali ngumu za kikazi yalikuwa miaka mingi kabla ya ujio wa Mapinduzi ya Viwandani kufanyika. Jamii ya kabla ya viwanda haikuwa na mabadiliko mengi na mara nyingi ilikuwa na uhasama mwingi—watoto kufanya kazi, hali hafu za maisha, na masaa marefu yalikuwa kwa wingi hata kabla ya Mapinduzi ya Viwandani.
Nimeelezea kwa kirefu hatua mbalimbali za mapinduzi ya viwanda huko ulaya ili uamini kwamba hata sisi watanzania tunaweza kabisa, waingereza wa karne ya 15 waliweza na Ng’ombe wao akazaa mapacha,inakuwaje kwetu wasizae?
Mwandishi, Fidelis Butahe   aliwahi kusema kwamba, huwezi   kuiweka Tanzania   katika kundi la nchi  maskini zaidi duniani hata siku moja. Kwa maana kwamba Ng’ombe wa maskini naweza akazaa tena uzao wake unaweza kuwa mapacha na kumshangaza mfugaji. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ina utajiri mkubwa wa rasilimali, ingawa wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa. Swali la kujiuliza hapa ni je tatizo ni nini? Utangundua kwamba tukiachana na imani potofu Ng’ombe wetu atazaa mapacha.Na ndivyo ilivyo kwenye ujasiriamali weka mikakati ya aina ya ujasiriamali unaotaka na Ng’ombe wako atazaa mapacha.

Tatizo kubwa letu na penginepo duniani  ni kuwa, na baadhi ya viongozi hasa wale  wa kisiasa na watu wa kada ya kati (middle class) na wananchi ni kuwa na imani potofu na kujilisha imani za kimasikini kwamba pasipo ajira hakuna kinachofanyika.
Juzi usiku kuna msomaji wa makala ya uchumi na biashara aliniambia kwamba, watu wanaojiita wasomi,nivigumu sana kufanya biashara za kisomi kwasababu wao niwaoga wa kuthubutu mambo, wanashindwa kujaribu.Alienda mbele kwa kusema kwamba, hapa Iringa mjini makampuni mengi, na majengo makubwa yanamilikiwa na watu ambao hajasoma  ama wana elimu tu ya kawaida.
Maggid Mjengwa ambae ni ‘mentor’ wangu alipata kusema kwamba,  “Tumekuwa watu wa kulalamika sana. Na tumemwachia Mungu jukumu la kutukomboa kutoka kwenye umasikini wetu. Hapana, Mungu hausiki na umasikini wako, unaosababisha Ng’ombe wako asizae. Jukumu la kwanza la kujikomboa kutoka kwenye umasikini ni lako mwenyewe. Tumeendekeza imani potofu zilizozagaa mitaani za Free mason na zinazoandikwa kwenye magazeti ya udaku kila leo
 Na hakuna njia ya mkato, bali ni kufanya kazi, kufanya kazi na kufanya kazi. Tufanye mapinduzi kama waingereza wa miaka hiyo. Achana na ndoto za kuamka na kuvuna mamilioni.Inakuwaje mwanadamu mmoja awe na muda na mwingine asiwe nao? Kuwa au kutokuwa na muda, inatokana na mipangalio yako ya maisha. Binadamu unapaswa kuwa na bajeti ya muda wako.

Ni jinsi unavyotumia muda wako, jinsi unavyopangilia mambo yako, imani yako kuhusu pesa,kushabikia siasa za marekani na michezo ya kuigiza na mambo mengine ya kufikirika, kuliko mambo,  mwisho wa siku unaishia kutamka kauli tata za NG’OMBE WA MASKINI HAZAI, sasa kama halishwi na hatunzwi atazaa kweli?  Jiulize.
 Maisha ni magumu sawa,mifumo ya nchi ni mibovu sawa,uchumi wa nchi unaporomoka sawa lakini haiwezi kuwa na madhara katika roho ya binadamu aliyeamua maisha yake.
Mambo ni mengi yanayoweza kuturudisha nyuma lakini ukirudi nyuma ni maamuzi yako wewe na si mambo yanayokuzunguka.
Au kiongozi wako wa kisiasa.

                                Mawasiliano: meshackmaganga@gmail.com
Previous
Next Post »