Hivi karibuni mwimbaji wa Marekani Kelly Rowland alivishwa pete na mchumba wake Tim Witherspoon ambaye pia ni meneja wake, na wanatarajia kufunga ndoa siku zijazo. Kelly ambaye alikua ni member wa kundi la kina dada watatu Destinys Child, amedai kuwa harusi yake itakuwa ni ya watu watatu tu yaani yeye mumewe mtarajiwa na pasta.
Kwa kauli hiyo ya Kelly (32), wawili hao wanaonekana hawana mpango wa kualika mtu yeyote wa ziada, hata waliokuwa members wenzake wa kundi la Destinys Child, Beyonce na Michelle? Hilo ni swali watu wangi wamekua wakijiuliza toka atoe tamko hilo, japo hakutamka moja kwa moja kuhusu kutomualika Beyonce na Michelle.
Moja ya sababu ya Kelly na mchumba wake kutohitaji harusi kubwa na ya watu wengi ni kuwa ndoa ni ya wao wawili hivyo wanadai hawaoni sababu ya kualika watu huku watakaokuwa kwenye ndoa ni wao.
“I think we just really want it to be us and our pastor. That’s it, I mean, we are the only two that’s going to be in the marriage.” ,” Alisema Kelly.
Kelly aliongeza kuwa bado hawajapanga tarehe ya harusi yao.
EmoticonEmoticon