Hali ya winga wa zamani Edibily Lunyamila inaendelea vizuri,leo hii asubuhi mwandishi amepita kwenye hospitali ya Mwananyamala na kukuta Jopo la madaktari saba akiwemo Daktari bingwa wa tiba za michezo,Dr Mwankemwa wakimshughulikia vizuri mgonjwa huyo.
Pia leo asubuhi wachezaji kadhaa wa zamani kama vile Silvatus Ibrahim,Mohamed Hussein na Vincet Peter walipita kumjulia hali mwenzao,Hapo jana uongozi wa Klabu ya YANGA ulifika hospitalini pale ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Abdallah Bin Kleb,Nahodha wa zamani Ally Mayai na walipanga asubuhi ya leo wamwamishie kwenye hospitali ya Muhimbili,aliyepewa jukumu hilo alikuwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ndugu Mohammed Binda.
'' Jana viongozi wa Yanga tulikubaliana leo tumwamishie hospitali ya Muhimbili lakini tulipofika leo asubuhi madaktari wa hospitali ya Mwananyamala walitusihi tumwache kwanza kwani walikuwa tayari wanamshughulikia,kutokana na huduma nzuri aliyokuwa anapewa na madaktari wa hapa tumeonelea tumwache kwanza'' alinukuliwa Binda akielezea hali ya mgonjwa.

SOURCE:SHAFFIH DAUDA
EmoticonEmoticon