Mtayarishaji wa muziki, C9 ambaye amefungua studio yake binafsi hivi karibuni amesema ana mpango wa kuzunguka mikoani kutafuta wasanii wenye uwezo mzuri wa kuimba ili awasainishe kwenye label yake.
C9 ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa zoezi hilo litafanyika mwaka ujao na kwamba hataki kuwasaini wasanii wenye majina makubwa katika label hiyo.
“Ntaiandaa tour ya kupita kila mkoa kutafuta msanii ambaye ataweza kushinda na kuwa label, kwa hiyo wasanii ambao wanachipukia wakae tayari. Sitasaini na msanii mkubwa, mi naanza na msanii mdogo.” Amesema C9.
Amesema tour hiyo itaitwa C9 Tour ambayo itaanza mwezi wa tano mwakani na itachukua mwezi mmoja
EmoticonEmoticon