BBC yapeleka timu ya watu 140 Afrika Kusini kuripoti habari za msiba wa Nelson Mandela, watazamaji wa UK wailalamikia kwa kupendelea zaidi habari za Mandela

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail wa Uingereza, shirika la habari la BBC lilipeleka timu ya watu 140 nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuripoti matukio ya msiba wa Nelson Mandela, ikiwa ni pamoja na tukio kubwa na la kihistoria  la ‘memorial service’ iliyofanyika jana (December 10) kwenye uwanja wa mpira wa FNB ulioko Johannesburg, na kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali.
Pamoja na kazi nzuri ya kuripoti live tukio la jana, shirika hilo limepokea jumla ya malalamiko 1350 kutoka kwa raia wa Uingereza, waliodai kuwa shirika hilo limeweka kando matangazo ya ndani (Uingereza) na kutumia muda mrefu kuripoti kuhusu msiba wa Nelson Mandela.
Shirika hilo limetetea uamuzi wake wa kuripoti matukio ya msiba wa Madiba kwa kusema taarifa za kifo chake zilikuwa na maslahi makubwa zaidi kwa watazamaji, wasikilizaji wa wasomaji wake wa Uingereza na duniani kwa ujumla.
Msemaji wa BBC aliiambia Daily Telegraph, “Katika kipindi cha siku kumi tutakuwa tumepeleka waandishi wapatao 120, mafundi mitambo, na wafanyakazi wa kusaidia katika habari hii kubwa ya kimataifa”.
Previous
Next Post »