TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.11. 2013





WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                   MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 17.11.2013  MAJIRA YA  SAA 11:30HRS HUKO  KATIKA KIJIJI CHA IGAWA, KATA  YA  LUGERERE,   TARAFA YA  RUJEWA,  WILAYA YA  MBARALI  MKOA WA MBEYA, GARI DS 7860/NN9  AINA YA  NISSAN TANKER  LIKIENDESHWA NA DEREVA MILLA S/O FERNANDO,  MIAKA 38, RAIA NA MKAZI WA NCHINI MALAWI LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  FITA S/O MAKOWO,  MIAKA 30,  MBENA, MKULIMA MKAZI WA KIJJI CHA IGAWA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   MADEREVA KUWA MAKINI  WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  




[DIWANI ATHUMANI- ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


NYONGEZA YA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.11. 2013.

      WILAYA YA MBEYA MJINI – UTAMBUZI WA MADAWA YA KULEVYA YALIYOPATIKANA
                                                         KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.

·         MNAMO TAREHE 15.11.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DSM ULIFANYIKA UCHUNGUZI WA KITAALAM KUHUSIANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA YALIYOKUTWA KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.

·         MADAWA HAYO YALIPOPIMWA AWALI YAKIWA KATIKA MUUNDO WA PIPI ZIPATAZO 65 NA MOJA IKIWA IMEPASUKA ZILIZOVINGIRISHWA KWA KUTUMIA NYLON MAALUM YALIKUWA NA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140. HATA HIVYO KATIKA UCHUNGUZI HUO MADAWA HAYO YALIBAINIKA KUWA  NA UZITO WA GRAM 972. 85 IKIWA NI BAADA YA KUYATOA MADAWA HAYO KATIKA NYLON MAALUM HIVYO UZITO WA NYLON MAALUM PEKEE NI GRAM 167.15 NA YALIBAINIKA KUWA NI AINA YA HEROINE.

§  AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM S/O SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

§  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.

§   BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA. WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 TUMBONI.

§  MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID S/O ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN S/O SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA  MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM. BAADA YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA  ALIKUWA  ANAITWA KASSIM S/O SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.

§  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI  KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.



[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »