NINI KIPO NYUMA YA HIZI MASHINE ZA TRA




milangoo

Wafanyabiashara mbalimbali wa kariakoo leo wameingia kwenye Mgomo kuishinikiza serikali kupunguza bei ya mashine za TRA ambazo zipo kwa ajili ya kutoa risiti.

Mashine hizo ziitwazo Electronic Fiscal Device[EFD] wamezigomea wakidai zinauzwa bei kubwa na sababu nyingine ni ile asilimia inayokatwa kwenye kila bidhaa inayouzwa ambayo ni asilimia 18%.
sideee

Huyu ni mmoja kati ya wafanyabiashara wa kariakoo ambaye pia ni msanii wa Bongo fleva anaitwa sideboy.
lilofunguliwa

Katika pitapita zangu hili ni duka pekee nililolikuta wazi kwenye barabara ya uhuru lakini niliporudi mara ya pili muda mfupi nikakuta limefungwa.
home shoping centre

Hili duka la Home shopping centre lipo barabara ya Uhuru nalo lilikuwa limefungwa.
wakongoWafanyabiashara mbalimbali wakiwemo raia wa nchi ya Congo hapa.
wafanyabiashara wakijadili
Hapa ni Wafanyabiashara wakiwa wanajadili kuhusu huu mgomo ambao haujajulikana utaisha lini.

picha zote zimepigwa na millardayo.com
Previous
Next Post »