WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 12.11.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISECHE KATA YA MWAMBANI,
TARAFA YA KWIMBA WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA, SILVESTER S/O ALPHONCE CHIKONDO, MIAKA
55, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISECHE ALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA RUNGU KICHWANI UTOSINI PAMOJA NA NGUMI NA MKE WAKE HUSULINA D/O KORNEL MIAKA 42,
MNYAMWANGA, MKULIMA, AKIWA NA MTOTO WAKE KONDO
S/O SILVESTER ALPHONCE CHIKONDO, MIAKA 19, MNYAMWANGA, MKULIMA WOTE WAKAZI
WA KIJIJI CHA ISECHE. MBINU NI
KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA BAADA YA KUFIKA
NJE YA NYUMBA WAKITOKEA KILABU CHA POMBE
ZA KIENYEJI. CHANZO NI WIVU WA
KIMAPENZI KUFUATIA MAREHEMU KUONGEA NA MWANAMKE MWINGINE WAKATI WAKIWA
KILABUNI. BAADA YA KUPIGWA MAREHEMU ALIANGUKA KISHA KUFARIKI DUNIA, WATUHUMIWA
WALIKIMBIA MARA BAADA YA KUGUNDUA MHANGA
AMEFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUBAINIKA UBONGO
KUCHANGANYIKA NA DAMU HIVYO KUSABABISHA KIFO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA
WITO KWA JAMII HASA WANANDOA KUTATUA MATATIZO / KERO ZAO KWA NJIA
YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO NA KUJENGA HOJA BADALA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI/KUTUMIA
NGUVU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA PIA
KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,
VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon