Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili
wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu na vya Ufundi Stadi ambao majina
yao yanapatikana katika tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania, www.policeforce.go.tz
Orodha ya majina hayo itapatikana pia
katika Gazeti la habari Leo la
tarehe 04/11/2013.
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi [02:00] hadi saa kumi jioni [10:00] kila siku kwa taaluma/fani na
katika maeneo yafuatayo;
·
Fani za Menejimenti ya Rasilimali Watu,
Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia,
Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa,
Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na
Utunzaji Kumbukumbu. Usaili wa fani hizi utafanyika katika chuo cha
Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa
Kurasini Dar es salaam .
·
Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and
Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari
Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa
Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi
Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
·
Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya
kikosi cha
Ufundi yaani TEHAMA KEKO chini.
- Fani
ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi
cha Polisi
Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
- Wataalam
wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo
kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
Muhimu:
(i)Mwombaji afike kwenye usaili akiwa na
nakala halisi pamoja na vivuli vya vyeti vyote vya Masomo/Taaluma
[Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani kidato cha nne, sita ,Chuo
na cheti cha kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
(ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia
gharama za upimaji afya shilingi
elfu kumi (10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la
usaili.
(iii)Kwa kuwa muda ni mchache anaekuja
kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa atapelekwa katika
Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani
tarehe 19/11/2013.
EmoticonEmoticon