Mahakama
ya rufani Tanzania imeanza kusikiliza rufaa ya mwanamuziki maarufu Tanzania
Nguza Viking (Babu Seya) na mwanae Johnson Nguza (Papii Kocha) ambao
wanatumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji na
ulawiti wa watoto.
Katika
rufani hiyo iliyosikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani ambao
ni Mbarouk mbarouk, Salum Massati na Nathalia Kimaro, wakili wa upande wa
mashtaka Mabele Marando amesema amekata rufaa kutokana na kutosikilizwa kwa
shahidi muhimu kwenye kesi hii ambae alitajwa kuwa ndie aliwapeleka watoto hao
kwa babu Seya.
Marando
amesema pia ushahidi wa kuunga mkono ushahidi uliotolewa na watoto
haukuzingatia sheria baada ya mahakama kutembelea nyumbani kwa babu Seya na
kumuhoji mtoto bila ya kiapo hivyo ameomba Mahakama ipitie upya hukumu hiyo ili
kurekebisha kasoro zilizojitokeza.
Baada
ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, wakili wa serikali Jackson Bulashi akiwa na
wenzake wanne amepinga maombi yaliyotolewa na upande wa mlalamikiwa na
kubainisha kwamba hoja zilizowasilishwa Mahakamani zilipaswa kuwasilishwa awali
wakati kesi hiyo ilipokua inasikilizwa.
Wakili
huyo wa serikali ameiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo kutokana na
kutoainisha athari za moja kwa moja kwa washitakiwa na kutaka adhabu ya kifungo
cha maisha iliyotolewa dhidi ya babu Seya na Papi Kocha iendelee kutekelezwa.
Baada
ya pande zote mbili kutoa maelezo yao mbele ya jopo la majaji watatu,
Mwenyekiti wa jopo hilo Jaji Nathalia Kimaro ameahirisha kesi hii ili kutoa
nafasi kwa majaji kupitia maelezo yote yaliyotolewa na kuyatolea maamuzi.
Mwaka
2004 Babu Seya na wanae watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela na hakimu
mkazi Addy Lyamuya wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo
baada ya hukumu hiyo, February 2010 walikata rufaa Mahakama kuu ya Tanzania
ambayo iligonga mwamba mbele ya jaji Thomas Mihayo wa Mahakama hiyo.
Jopo
la majaji lililosikiliza rufaa hiyo ndilo lililosikiliza awali na kuwaachia
huru watoto wawili wa Babu Seya ambao ni Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya
kuonekana hawakuwa na hatia.
EmoticonEmoticon