TFDA yateketeza samaki wa mamilioni




Afisa Habari wa TFDA, Gaudensia Simwanza


Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imewateketeza samaki waliooza  aina ya vibua wenye thamani ya Sh. milioni 11.4 walioingizwa nchini na kampuni ya Sais Boutique. 

Samaki hao walioingizwa kutokea China na TFDA iliwakamata katika eneo la Tabata Bima wakati wa ukaguzi wa bidhaa za chakula.

Afisa Habari wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliyasema hayo alipokuwa akizingumza na NIPASHE na kuwa ukaguzi huo uliofanyika Septemba 18, mwaka huu wakati zoezi hilo linaendelea waliwabaini samaki hao kuwa wameoza na hawafai kwa matumizi ya binadamu.

Aidha, Simwanza alisema mmiliki wa kampuni ya Sais tayari alichukuliwa hatua ya kufunguliwa kesi mahakani yenye kumb.namba BUG/RB/1184/2013 kwa kosa la kuhifadhi samaki waliooza na alihukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni moja na kuteketeza  mzigo huo kwa gharama zake.

Previous
Next Post »