·
JANA TAREHE 01/10/2013 KATIKA UKUMBI WA
MTENDA MHE. ABBAS KANDORO, MKUU WA MKOA AKIWA NA MAOFISA WA TRA WALIKUTANA NA
WAFANYA BIASHARA KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZILIZOPO KATIKA ENEO LA
BIASHARA.
·
KUTOKANA NA MJADALA HUO MHE. MKUU WA
MKOA AMEANZA KUFUATILIA KUPATA MAJIBU/UFUMBUZI TOKA NGAZI ZA JUU KWA BAADHI YA CHANGAMOTO ZILIZOTOLEWA.
·
JIONI YA JANA 01/10/2013 KAMANDA WA POLISI PIA ALIKUTANA NA
VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA AMBAPO BAADA YA MJADALA VIONGOZI HAO WA
WAFANYA BIASHARA WALIONA UMUHIMU WA KUAHIRISHA MKUTANO ULIOTANGAZWA KUFANYIKIA
UWANJA WA RUANDA NZOVWE KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA KI-USALAMA.
·
ZIPO TAARIFA ZA KUWEPO BAADHI YA
WATU WAKOROFI WASIO VIONGOZI, WANAOPENDA
VURUGU WANALAZIMISHA WATU WAFUNGE BIASHARA, WANANCHI TUSIWAKUBALI WATU HAO WANA
NIA YA KUVURUGA AMANI.
·
UKIWA NA TAARIFA YA MKOROFI
YEYOTE/MVUNJAJI AMANI ITOE POLISI HARAKA.
TANGAZO LIMETOLEWA NA: DIWANI ATHUMANI-ACP
KAMANDA
WA POLISI
MKOA WA MBEYA
EmoticonEmoticon