WILAYA YA ILEJE – MAUAJI.
|
MNAMO
TAREHE 01.10.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IZUBA WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. SIKWITA D/O NAMWOVE, MIAKA 70, MLAMBYA, MKULIMA,
MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA MOHAMED S/O MWAMAHONJE, MIAKA 36,
MKULIMA, MLAMBYA, MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA. MBINU NI KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA JIKONI NYUMBANI KWAKE NA KUMUUA. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA
ANAMLOGA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA
KISHIRIKINA KWANI ZINALETA MADHARA
MAKUBWA KATIKA JAMII.
WILAYA YA MBEYA MJINI
– KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE
01.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS
HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA MOSES S/O
SAID MIAKA 17, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA ITIJI AKIWA NA BHANGI KETE 14
SAWA NA UZITO WA GRAM 70. MBINU NI
KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA YA KUUZA SIGARA.
MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon