TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15. 09. 2013.




WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI {GONGO}



MNAMO TAREHE 14.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:20HRS HUKO KITONGOJI CHA KISUNGU KIJIJI CHA UPENDO KATA YA   MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOANI MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIMKAMATA FELISTA D/O ROMAN, MIAKA 36, MNYAMWANGA, MKULIMA NA MKAZI WA KIIJIJI CHA KISUNGU AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] LITA 12 KATIKA DUMU LA LITA 20, MBINU ILIYOTUMIKA NI KUIFICHA NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO.    MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA MARA MOJA TABIA YA  KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA .



WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI

MNAMO TAREHE 15/09/2013 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO ITUHA JIJINI MBEYA WATU WAWILI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA SOPHIA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI MIAKA 35 – 40, MSAFWA, MKULIMA NA MKAZI WA ITUHA, PAMOJA NA MTU MMOJA MWANAUME AMBAYE HAJATAMBULIWA, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 40 – 45 WALIFARIKI DUNIA WAKATI WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA MAWE NA MARUNGU SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUWAVAMIA WAKIWA NJIANI WAKIREJEA NYUMBANI USIKU. CHANZO CHA MAUAJI HAYO KINAHUSISHWA NA WIVU WA KIMAPENZI,HADI SASA MTU MMOJA  AITWAE  ZEBEDAYO S/O JOHN, MIAKA 32, MSAFWA, MKULIMA NA MKAZI WA ITUHA AMEKAMATWA KWA KUTILIWA MASHAKA KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA UPELELEZI UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WATUMIE NJIA YA  MAZUNGUMZO KUMALIZA MIGOGORO YAO. PIA ANATOA RAI KWA WANANCHI/YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WAHUSIKA WA TUKIO HILO WAZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.          





 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »