TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 10. 09. 2013.





          WILAYA YA  MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                                   MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 09.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS HUKO ENEO LA UYOLE STENDI YA USANGU BARABARA YA  MBEYA/IRINGA JIJI NA  MKOA WA  MBEYA. GARI T.403 AAS AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA SADICK S/O NYAHI MIAKA 38, MBENA, MKAZI WA MAMA JOHN LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI  YAKE  JINSI YA  KIUME MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 33-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. CHANZO NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA  MBEYA MJINI  – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.

MNAMO TAREHE 09.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA AIRPORT JIJI  NA  MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA CHARLES S/O EWIMA, MIAKA 24,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA AIRPORT AKIWA NA MICHE MINNE YA  BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 78. MBINU NI KUHIFADHI  MICHE HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 


 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »