Zuma ampa hongera kubwa Mugabe

Zuma akikaribishwa na Mugabe alipozuru Harare zamani

 

Rais Zuma amesema uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ulifanikiwa, na ametoa wito kwa pande zote zikubali matokeo.

Mpinzani mkuu wa Bwana Mugabe, Morgan Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 61, amekataa matokeo na amesema atapeleka malalamiko mahakamani.

Viongozi wa mataifa ya magharibi yamesema yana wasi-wasi kama uchaguzi ulikuwa wa halali.

Bwana Mugabe alipata asili-mia-61 ya kura katika uchaguzi wa rais.

Na chama chake cha ZANU-PF kilipata thuluthi mbili ya viti vya bunge.

Previous
Next Post »