Bunge la Uruguay limepitisha
mswada wa kuhalalisha bangi. Ikiwa mswada huu utapitishwa na Baraza la
Senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha uzalishaji na
utumiaji wa bangi.
Hatua hii inaungwa mkono na serikali ikisema
itapunguza mapato na faida kubwa kwa walanguzi wa mihadarati pamoja na
kuwafanya watumizi wa bangi kutotumia dawa kali za kulevya.Chini ya
mswada huo ni serikali pekee itakua na kibali cha kuuza bangi.
Pia serikali itatoa utaratibu wa uzalishaji,
mavuno, uhifadhi na mauazo ya nje. Wanunuzi wote watanakiliwa kwenye
daftari maalum na sharti wawe wametimiza miaka 18 na zaidi. Mteja
anaweza tu kununua kilo 40 kwa mwezi kutoka kwa maduka ya dawa au kukuza
mimea sita ya bangi.Wageni hawatakubaliwa kununua bidhaa hii.
Wabunge 50 kati ya 96 walipitisha mswada huo.
Wanaotetea kuhalalishwa kwa bangi wamesema vita dhidi ya mihadarati
havijapiga hatua na ipo haja kuweka mbinu mpya.
Kwa miongo mingi kanda ya Latin America
imekumbwa na ghasia za magenge ya mihadarati ambapo maelfu ya watu
wamekufa. Matukio ya Uruguay yanatazamwa kwa karibu eneo hilo ikiwa
yatasaidia kupunguza machafuko yanayotishia uthabiti wa mataifa mengi.
EmoticonEmoticon