Nyota wa muziki na waigizaji filamu wa nchini Nigeria wakiwemo P-Square, 2Face, Omotola, Yvonne Nelson, na wengineo wengi wanatarajia kuonekana katika tuzo maarufu za African Oscars za mwaka huu ambazo zitatolewa tarehe 14 mwezi Septemba.
Sherehe kubwa kabisa za ugawaji wa tuzo hizi zitafanyika huko Washington DC Marekani ambapo waandaaji wakubwa wa mpango huu mzima ni timu ya wakosoaji filamu za Nollywood na Afrika kwa ujumla kutoka USA.
Wasanii mbalimbali wanaotarajiwa kuvuta macho ya wengi katika siku hii kubwa ni pamoja na Omotola Jalade-Ekeinde, Yvonne Nelson, Uche Jombo-Rodriguez pamoja na 2face Idibia na kundi la P-Square kwa upande wa wanamuziki.
EmoticonEmoticon