NYONGEZA YA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 09. 08. 2013




   WILAYA YA KYELA -    WATUHUMIWA SITA WADHIBITIWA NA WAUMINI KWA  USHIRIKIANO NA MAKACHERO WA POLISI WALIPOTAKA KUANZISHA FUJO.

 MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO ENEO LA BONDENI KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. NURU S/O MWAFILANGO,MIAKA 77,KYUSA,SHEKHE MKUU WA WILAYA YA  KYELA, MKAZI WA BONDENI  AKIWA ANAONGOZA IBADA YA  SWALA YA    IDD EL FITRI  MSIKITINI HAPO ALIVAMIWA NA BAADHI YA  WAUMINI WANAOJIITA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUTUMIA FIMBO,NONDO,MKASI NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. CHANZO NI MADAI KUWA HAWAMTAKI SHEKHE HUYO KWA MADAI KUWA HANA UWEZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA WAKATI WAUMINI WOTE WAKIWA  WAMEINAMA WAKISWALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA. MHANGA HAKUPATA MADHARA BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKIANA NA POLISI/MAKACHERO WA-KIISLAMU KUMUOKOA.   KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA SITA AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1.MASHAKA S/O KHASIMU,MIAKA 30,MUHA,MKULIMA MKAZI WA NDANDALO 2. ISSA S/O JUMA, MIAKA 37, MRANGI, MKULIMA,MKAZI WA BONDENI 3.AHMED S/O KHASIMU @ MAGOGO,MIAKA 35,MPOGORO,MKULIMA/MGANGA WA KIENYEJI, MKAZI WA MBUGANI [ALIKUTWA NA MKASI] 4. IBRAHIM S/O SHABAN,MIAKA 17,KYUSA,MWANAFUNZI SHULE YA  SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA NNE MKAZI WA NDANDALO [ALIKUTWA NA FIMBO KUBWA NA NDIYE ALIYEMNYANG’ANYA SHEKHE KIPAZA SAUTI] 5. AMBOKILE S/O MWANGOSI @ ALLY,MIAKA 19,KYUSA,MWANAFUNZI WA SHULE YA  SEKONDARI  KYELA DAY KIDATO CHA TATU, MKAZI WA BONDENI [ALIKUTWA NA KIPANDE CHA NONDO] NA 6. SADICK S/O ABDUL, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NDANDALO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KATIKA TUKIO HILO HAMIS S/O
HUSSEIN, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI ALIPATA MAJERAHA KIDOGOKWA  KUKATWA MKASI  JUU YA  SIKIO LA KUSHOTO WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMUOKOA MHANGA ASIPATE MADHARA  NA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.  HALI  YA  USALAMA NA AMANI  ILIREJEA MUDA MFUPI NA   WAUMINI WALIENDELEA NA IBADA YAO CHINI YA  UONGOZI WA SHEKHE HUYO NA KUMALIZA SALAMA. HAKUNA UHARIBIFU WA MALI ULIOTOKEA .KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAUMINI NA JAMII KWA UJUMLA KUTATUA MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA   KUKAA KWENYE  MEZA YA  MAZUNGUMZO BAADA YA   KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANASISITIZA  KUWA KWA YEYOTE ATAKAYEJARIBU /ATAKAYEVUNJA SHERIA HATAFUMBIWA MACHO.
   Imesainiwa na,
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »