RAIS
Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji
wa Serikalini kwenye nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika
wizara mbalimbali, ambapo wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine
na yumo anayestaafu.
Kauli
hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais
amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za
Serikali katika ngazi hizo za juu,”alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko
yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk. Florens
Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara
ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki(awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda,Biashara na Masoko, Jumanne Sagini amekuwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) awali
alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Wengine
ni Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,awali
alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha, Dk. Patrick Makungu amekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya
Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Dk.
Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Dk.Uledi Mussa
amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu
Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
Wanaofuata
ni Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali
alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri, Anna Maembe amekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu wizara hiyo, Sihaba Nkinga amekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara hiyo na Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Balozi
Sefue aliongeza kwamba Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho ni Peniel
Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu kwenye
‘Presidential‘s Delivery Bureau’ kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la
kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
Makatibu
wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Kijakazi Mtengwa
aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto na Injia
Omari Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi.
Kwa
upande wa Makatibu wanaostaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amestaafu kwa hiari.
Aidha
Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu
wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao.
Alisema
naibu makatibu wakuu wapya walioteuliwa ni Angelina Madete
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Regina Kikuli Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Zuberi Sumataba Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu – TAMISEMI- anayeshughulikia suala la elimu katika ngazi
za Serikali za Mitaa , Edwin Kiliba Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Wengine
Deodatus Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI ambaye
atashughulikia saula la afya upande wa Serikali za Mitaa, Dk.
Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika, Profesa Adolf Mkenda Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia
sera, Dorothy Mwanyika Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni.
Rose
Shelukindo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.
Selassie Mayunga Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Monica Mwamunyange Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,
Consolata Mgimba Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
Naibu
makatibu wakuu wengine ni Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Armantius Msole
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi
Sefue aliwataja naibu makatibu wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni John Mngondo
ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo, Selestine Gesimba
amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii anatoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na
Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais.
Wanaofuatia
ni Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Nuru Milao anahamia Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
EmoticonEmoticon