MWANAMKE AMPIGA MPAKA KUMUUA MTOTO WA MIAKA MITATU KISA TU KATAPIKA
Mwanamke mwenye miaka 21 Rebecca Bassey, amekamatwa na na polisi huko Lagos kwa tuhuma za kumpiga mtoto ambaye ni mpwa wa mumewe mwenye umri wa miaka mitatu Deborah Bassey, na kumsababishia kifo chake.
Kwa mujibu wa polisi anasema mtuhumiwa alimpiga hadi kufa binti huyo kwa sababu alijitapikia .
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Ijaiye Ojokoro siku ya Alhamisiwa Julai 22, 2013.
Deborah alimpoteza mama yake mwaka 2010 ambapo alifariki hivyo mapema mwaka huu baba yake aliamua kumpeleka Deborah kwa mdogo wake sababu alikuwa amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na kuamua ni vyema ampeleke mwanae kwa ndugu yake Vicent mpaka atakapo seto kimaisha ili asipate shida na yametokea ya kutokea jamani hivi huu ukatili kwa watoto utaisha lini..
EmoticonEmoticon