Maajabu
mengi sana hugundulika duniani kila siku lakini kuna kila uwezekano
kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee manake
Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki
serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu
Kristo.
Mwanasheria
huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The
Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na
Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria
huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa
kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya
Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia
yoyote ya kustahili adhabu hiyo .
Dola
Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa
Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo
Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo
mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua
Bwana Yesu .
Indidis
anasema kuwa ushahidi uko kwenye kitabu kitakatifu Cha Biblia ambayo
kila mmoja anafahamu kuwa haisemi uongo . Kwa kuwa wafalme na watawala
waliohusika na kitendo hicho hawako hai serikali ambazo mipaka yake ndio
ile ile ya iliyokuwa falme ya Roma iliyokuwa madarakani kipindi hicho zitawajibika kwa niaba .
Dola
Indidis anasema kuwa vitendo alivyofanyiwa Yesu ni vitendo vya kinyama
na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nay eye kama mwanadamu
anahisi kuwa ni jukumu lake kulinda na kutetea heshima ya Yesu Kristo.
Hata
hivyo msemaji wa mahakama ya Dunia ambaye hakutajwa utambulisho wake
amesema kuwa hakuna kipengele cha kisheria ambacho kinaweza kuruhusu
kusikilizwa kwa kesi hiyo kwani ICJ (International Court Of Justice)
husikiliza kesi zinazohusu nchi dhidi ya nchi nyingine hivyo
kesi hiyo haiwezi hata kufikiriwa . Indidis kwa upande wake bado ana
imani kuwa ana kesi ya kuhoji na anaamini kuwa atashinda kesi hiyo.
EmoticonEmoticon